Thursday, February 4, 2016
ZANZIBAR WATAKIWA KUHAKIKI SIMU ZAO HARAKA ILI KUKWEPA KUFUNGIWA IFIKAPO MWEZI WA 7
Do you like this story?
Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka Wazanzibari kuhakiki simu zao za mkononi
ili kuepuka kufungiwa mawasiliano ifikapo Julai, mwaka huu kutokana na sababu
mbalimbali ikiwamo ya kuwapo ambazo ni feki.
Akizungumza na
waandishi wa habari mjini Unguja jana, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent
Mungy alisema ni vyema wananchi wote kuhakiki simu zao ili wakati wa kufungia
zisizofaa wasikose mawasiliano.
Mungy alisema
TCRA imefikia uamuzi wa kutekeleza matakwa ya sheria kutokana na kuwapo kwa
vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa maadili kwa kutumia simu.
Alisema
kumekuwapo na utumiaji wa simu usio mzuri unaofanywa na baadhi ya wananchi,
ikiwamo baadhi yao kuzisajili kwa kutumia majina ya watu ili kuepuka
kutambulika wanaposhiriki uhalifu.
“Pamoja
na kuwapo kwa baadhi ya watu kusajili simu kwa maji na yasio yao, lakini pia
kumekuwapo na vitendo vya wizi wa simu. Hivyo tunaamini wazi kuwa njia hii kwa
kiasi kikubwa itasaidia jamii, kwani hata mtu akiiba simu kwa mujibu wa
taratibu zetu hataweza kuitumia,”
alisema.
Meneja huyo
alisema mfumo unaotarajiwa kutumika nchi nzima utamlazimisha mtumiaji wa simu
kutumia inayokubalika kisheria, huku usajili wake ukiwa hauna mashaka.
Alizitaja
baadhi ya njia ambazo mtumiaji wa simu atahitajika kuzizingatia kabla na baada
ya kununua kuwa ni kuhakikisha inalingana na mabadiliko ya kiteknolojia na
kupewa muda maalumu wa kutumia usiopungua miezi 12.
Naibu
Mkurugenzi wa Masuala ya Matumizi ya Mitandao wa TCRA, Thoday Ringo alisisitiza
haja ya wananchi kuwa makini kununua simu zenye ubora.
Alisema baadhi
ya watu wamekuwa wepesi kununua simu zinazouzwa kwa bei ya chini bila ya kujua
madhara yake.
“Napenda
kuwatahadharisha ndugu zangu kuepuka kununua simu ovyo, la msingi ujue kuwa
zipo ambazo ni feki,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ZANZIBAR WATAKIWA KUHAKIKI SIMU ZAO HARAKA ILI KUKWEPA KUFUNGIWA IFIKAPO MWEZI WA 7”
Post a Comment