Monday, November 10, 2014

MNIGERIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULENYA UWANJA WA NDEGE.


Madawa ya kulevya yakiwa chini kwenye sori ya kiatu



Tumekua tukizipata taarifa za watu mbalimbali kukamatwa na dawa za kulevya kwenye viwanja vya ndege pamoja na sehemu nyingine za kusafirishia ambapo kila mmoja amekua na mbinu yake kusafirisha mzigo huo haramu.

Taarifa kutoka  Nigeria ambapo mwanaume aitwae Mama Solomon kutoka Enugu amekamatwa kwenye uwanja wa ndege Lagos akiwa ameficha dawa za kulevya aina ya Cocaine katikati ya soli ya kiatu cha Mwanamke.

Jamaa alikua akitokea Brazil ambayo ni nchi maarufu sana kwa kuziuzia nchi nyingine dawa za kulevya na alikua na mifuko miwili iliyojaa viatu vya Wanawake na pochi.

Baada ya kukamatwa, Solomon mwenye umri wa miaka 27 alikataa dawa hizo kuwa za kwake na kusema yeye amekua akifanya kazi na kuishi nchini Brazil hivyo kuna rafiki yake alimpatia huo mzigo na kumwambia akiufikisha salama atazawadiwa.

0 Responses to “MNIGERIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULENYA UWANJA WA NDEGE.”

Post a Comment

More to Read