Saturday, November 15, 2014

TRA MKOA WA MBEYA YATARAJIA KUADHIMISHA SIKU YA MLIPA KODI.




Meneja wa TRA Mbeya Anord Maimu akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa maadhimisho ya siku ya Mlipa kodi  inayotalajiwa kaunza Nov 17 hadi 21 mwaka huu.


MAMLAKA ya Mapato TRA Mkoa Mbeya imewataka wafanyabiashara  kutambua kuwa suala la matumizi ya mashine za EFD lipo kisheria hivyo ni vema wakaitekeleza kuliko kuendelea kutupiana lawama.

Imesema, bunge ndio lililopitisha sheria hiyo na mamlaka  inawajibika katika usimamizi na utoaji wa elimu hivyo hakuna haja ya kuendelea na mvutano.

Kauli hiyo imetolewa  na Meneja wa mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mbeya, Anord Maimu, wakati akizungumza na waandishi juu ya kuadhimisha wiki ya mlipa kodi ambayo kila mwaa huadhimishwa na mamla hiyo.

Amesema, mamlaka haitungi sheria kwani sheria zote wanazozisimamia zimepitishwa na Bunge hivyo suala la mashine lililipitishwa na bungeni na wenye wajibu wa kulitekeleza ni TRA.

Amesema, kazi kubwainayofanywa na TRA ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine hizo pamoja na umuhimu wake katika kuinua pato la Taifa kupitia mashine hizo.

Amesema wao kama mamlaka hawana mvutao wowote na wafanyabiashara hao kama ambavyo imekuwa ikitafsiliwa na wengi badala yake wao wamekuwa mstari wa mbele katika kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya mashine hizo.


Aidha, Maimu aliwataka wafanyabiashara hao kuitumia vizuri siku ya mlipa kodi inayotarajia kuanza November 17 mwaka huu na kilele chake kufanyika November 21 katika ukumbi wa Mkapa.

Hata hivyo, alisema katika siku hiyo TRA inakusudia kufanya shughuli mbalimbali zilizoambatana na utoaji huduma kwa makundi muhimu ya jamii kama vile utoaji wa vyandarua 50 na shuka 50 katika hospitali ya Wilaya ya Kyela.

 

0 Responses to “TRA MKOA WA MBEYA YATARAJIA KUADHIMISHA SIKU YA MLIPA KODI.”

Post a Comment

More to Read