Tuesday, November 11, 2014

WALIMU WAWILI WAKAMATWA WAKITUHUMIWA KUVUJISHA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE.




Walimu wawili wa Shule ya Sekondari ya Embarway wanashikiliwa na polisi wilayani Ngorongoro wakituhumiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne ofisini.

Licha ya walimu hao kukamatwa pia waliokuwa wasimamizi  wa ndani wa mitihani kwenye shule hiyo, wameondolewa kutokana na uzembe.

Kaimu ofisa elimu wa Wilaya ya Ngorongoro, Chacha Megewa  alidai walimu hao, Jakob Jadie na Reginald Boniface, walikamatwa wakati wakifanya mtihani wa historia.

Alisema walikamatwa Novemba 5 walikamatwa na msimamizi mkuu wa mitihani, Faustine Bura baada ya kuingia ghafla katika ofisi ya mwalimu mkuu.

“Msimamizi alikuwa anafuata moja ya fomu ofisi ya mkuu wa shule, baadaye aliita polisi na kuwakamata,” alisema.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas jana hakupatikana kuelezea tukio hili, lakini polisi Kituo kidogo cha Ngorongoro ilithibitisha kukamatwa kwa walimu hao.

0 Responses to “WALIMU WAWILI WAKAMATWA WAKITUHUMIWA KUVUJISHA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE.”

Post a Comment

More to Read