Thursday, December 4, 2014
CHELSEA HAISHIKIKI LIGI KUU ENGLAND
Do you like this story?
Mzunguko wa 14 umekamilika kwa timu zote 20 za ligi kuu ya
England kushuka viwanjani.
Chelsea, wameendeleza wimbi la ushindi na kukataa katakata
kuzipa nafasi timu nyingine 19 kupunguza pengo la pointi lililopo kati yake na
timu hizo.
Sergio Aguero, mchezaji wa Manchester City akishangilia moja
ya magoli yake katika ligi kuu ya England
Chelsea imeendelea kuwa na tofauti ya pointi sita na Man
City inayoifuatia baada ya kuirarua Tottenham mabao 3-0, huku Manchester City
yenye pointi 30 ikiisasambua Sunderland magoli 4-1. Sergio Aguero ameifungia
timu yake ya Manchester City magoli mawili katika mchezo huo, huku Jovetic na
Zabaleta kila mmoja akifunga bao moja.
Magoli ya Chelsea yamefungwa na Hazard, Drogba na Remy.
Wachezaji wa Arsenal Santi Carzola akishangilia goli na
Alexis Sanchez
Mchezo mwingine wa Jumatano usiku, ulikuwa kati ya Arsenal
na Southampton wanaoshikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya
England. Mchezaji Alexis Sanchez ndiye aliyekuwa shujaa na kuwanyanyua vichwa
mashabiki wa Arsenal pale alipoifungia timu yake goli pekee katika mchezo huo
ikiwa ni dakika ya 89 ya mchezo, uliofanyika uwanja wa Emirates na hivyo
kujikusanyia pointi tatu muhimu kuelekea kileleni.Arsenal inashikilia nafasi ya
sita ikiwa na pointi 23, pointi 13 nyuma ya vinara Chelsea yenye pointi 36.
Everton na Hull City ziligawa pointi baada ya kufungana bao
1-1.
Hadi kufikia mzunguko huo wa 14, Chelsea inaongoza kwa
kujikusanyia pointi 36, ikifuatiwa na Man City yenye pointi 30, Southampton ni
ya tatu na pointi 26, Huku Manchester United kiwa nafasi ya nne na pointi 25 na
nafasi ya tano inashikiliwa na West Ham yenye pointi 24.Ivabaada
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CHELSEA HAISHIKIKI LIGI KUU ENGLAND”
Post a Comment