Thursday, December 4, 2014
AFCON 2015:MAKUNDI YA TIMU 16 YATAJWA
Do you like this story?
Upangaji wa
makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya
kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015 yamefanyika katika mji mkuu
wa Equatorial Guinea, Malabo.
Mashindano hayo yataanza Januari 17, 2015.
Upangaji wa makundi ulirudishwa wiki moja nyuma ili
kuiwezesha Equatorial Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua nafasi ya Morocco,
iliyokuwa iandae mashindano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo baada ya
kutaka mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao
umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ambako zinatoka timu nyingi
zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni moja ya timu kubwa
zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani, pamoja na Misri na Angola
ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON 2015:
Kundi A Equatorial
Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo
Kundi B Zambia,
Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C Ghana,
Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D Ivory Coast,
Mali, Cameroon, Guinea
Wenyeji Equatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya
ufunguzi wa michuano hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana
na timu zilizopangwa kundi hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AFCON 2015:MAKUNDI YA TIMU 16 YATAJWA”
Post a Comment