fahari News
Habari | Michezo | Bishara | Zabuni
Home
BIASHARA
KITAIFA
KIMATAIFA
USA
AFRIKA
AFRIKA MASHARIKI
MICHEZO
MUZIKI
SIASA
Recommended:
Perfect Social Media Marketing Stratergy For Your Business
Like
Wednesday, December 3, 2014
UWEZO WA VYUO VIKUU KUCHUKUA WANAFUNZI WA SAYANSI BADO CHANGAMOTO KWA TANZANIA KUTIMIZA MALENGO YA EFA
Tweet
Share
Do you like this story?
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa akifungua mkutano wa kimataifa wa kutathmini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote-EFA uliofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo amesema tangu mwaka 2000 Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuelekea kutimiza malengo ya Mpango huo ikiwa ni utashi wa kisiasa na kuwajibika vikisaidiwa na kujitolea kwa wadau wa sekta ya elimu pamoja na washirika wa maendeleo.
Kamishna wa Elimu kutoka Wizarani, Prof. Eustella Bhalalusesa (wa pili kushoto) akitoa maoni juu changamoto zinazolikabili taifa katika kuleta uwiano kwenye ya sekta elimu.
Tanzania imekuwa moja wapo ya nchi za kutolea mfano miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara katika kutekeleza maazimio ya mpango wa Elimu kwa wote (EFA).
Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa wadau wote wa elimu , Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa amesema Tanzania Bara na Visiwani imeweza kukaribia kufikia malengo ya mpango huo ikiwa ni pamoja na suala la wastani wa waalimu kwa wanafunzi.
Amesema kwamba kwa shule za msingi Tanzania Bara imefikia wastani wa wanafunzi 47 kwa mwalimu mmoja wakati Visiwani Zanzibar ni wastani wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 27.
Mafanikio mengine yaliyopatikana chini ya mpango huo ni kuboresha wastani wa wanafunzi kwa darasa, ambapo kwa Tanzania Bara wastani umetoka kuwa wanafunzi 92 kwa darasa na sasa ni wanafunzi 65 huku Zanzibar wastani ukiwa ni wanafunzi 62 kwa darasa.
Awali Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues amesema ikumbukwe kwamba malengo nane (8) ya EFA yanachangia kufanikisha Malengo Makuu ya Maendeleo ya Millennia (MGDs) yaliyopitishwa mwaka 2000 kati ya nchi 189 na Taasisi za Mendeleo zinazoongoza Duniani.
Bi. Rodrigues amefafanua kuwa tunapoelekea mwaka 2015, Tanzania Bara na Visiwani zimeonyesha juhudi katika kupunguza tofauti kubwa zilizokuwepo kielimu ikiwa ni pamoja na kukabilia na changamoto zilizojitokeza na kuweza kuweka sera, mipango na utawala bora katia Nyanja za fedha , wadau, usimamizi na uwajibikaji.
Katika mkutano huo imeelezwa kwa sasa hakuna tatizo la uwiano wa wanafunzi wa kike na wa kiume kwa kuwa jinsia zote zipo darasani katika uwiano unaoridhisha unaokaribia wastani wa 50/50, lakini pia kigezo kingine ni uwiano wa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari ambapo bado kumeonyesha kuwa na mapungufu hivyo kazi ya ziada inahitajika.
Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na nia ya kutoa fursa kwa nchi wahusika kujitathimini zimefikia wapi katika utekelezaji wa malengo waliyojiweke ya Mpango wa Elimu kwa Wote-EFA kwa kipindi cha mwaka 2000 hadi 2015 na kujiwekea mikakati mipya.
(Picha na Zainul Mzige wa MOblog)
0 Responses to “UWEZO WA VYUO VIKUU KUCHUKUA WANAFUNZI WA SAYANSI BADO CHANGAMOTO KWA TANZANIA KUTIMIZA MALENGO YA EFA”
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tweets by @FahariNews
More to Read
Buzz
Twitter
Facebook
RSS
Email
Must Read
Popular Posts
MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA JESHI LA POLISI.
Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2013 na kidato cha sita mwaka 2014 ambao w...
NEYMAR KWAHERI COPA AMERICA, APIGWA PINI MECHI NNE NA FAINI YA KUTOSHA
Nyota wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar hatocheza tena michuano ya Copa America inayoendelea huko Chile baada ya kufungiw...
JULIO AWACHIMBA ‘MKWARA’ WANAOMLETEA MAGUMASHI
Kocha mkuu wa Mwadui FC Jamuri Kihwelo ‘Julio’ amewatolea uvivu wale wote ambao wamekuwa wakibeza mafanikio yake lakini wakidai peng...
YULE BIBI ALIYEKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR AANGUA KILIO MAHAKAMANI MPAKA HAKIMU AKAAHIRISHA KESI YAKE
Bibi wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole akipelekwa mahakamani. BIBI wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole (65), leo ameangua kilio...
WATANZANIA 7 WAMEUAWA KWA RISASI NCHINI ZAMBIA NA WATU WASIOJULIKANA.
Polisi wa Zambia wakibeba Miili ya watanzania Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi MIILI ya watu saba inayosadi...
0 Responses to “UWEZO WA VYUO VIKUU KUCHUKUA WANAFUNZI WA SAYANSI BADO CHANGAMOTO KWA TANZANIA KUTIMIZA MALENGO YA EFA”
Post a Comment