Wednesday, December 3, 2014
MASHINE YENYE UWEZO WA KUFIKIRI KITISHO
Do you like this story?
Profesa Stephen Hawking, mmoja wa wanasayansi
mahiri nchini Uingereza, amesema juhudi za kutengeneza mashine inayofikiria
inatishia uwepo wa binadamu.
Ameiambia BBC:"Kutengenezwa kwa mashine
yenye uwezo wa kufikiria inaashiria maangamizi ya binadamu."
Onyo la Profesa Hawking limekuja kutokana na
kuimarishwa kwa teknolojia anayotumia katika mawasiliano, ambayo inahusisha
msingi wa Akili Bandia(Artificial Intelligence, AI).
Lakini wengine hawana upinzani sana na
matarajio ya teknolojia hiyo ya AI.
Mwanasayansi huyo wa nadharia ya fizikia,
ambaye anaumwa ugonjwa wa mishipa ya fahamu (ALS), anatumia mfumo mpya
uliotengenezwa na kampuni ya Intel kuzungumza.
Wataalam wa mashine za kujifunza kutoka kampuni
ya Uingereza ya Swiftkey pia walihusika katika kunda mashine hiyo. Teknolojia
yao, tayari inatumika kama mfumo wa smartphone, unajifunza namna profesa
Hawking anavyofikiria na kupendekeza maneno ambayo huenda angetaka kuyatumia
baadaye.
Profesa Hawking amesema miundo duni ya akili
bandia (AI) ambayo imeboreshwa mpaka sasa imethibitisha kuwa na manufaa sana,
lakini ana wasiwasi wa madhara yanayotokana na kuunda kitu chenye uwezo sawa na
binadamu au kupita. "Mashine hiyo inaweza kujiwasha na kujizima na
kujibadili yenyewe katika kiwango kisichomithilika," amesema.
Cleverbot ni kifaa(software) ambacho kimeundwa
kuwasiliana kama binadamu anavyofanya "binadamu ambao wana ukomo wa
kufikiri kutokana na mabadiliko ya taratibu ya kibaolojia, hawawezi kushindana
na mashine hii, na watapitwa kwa mbali."BBC SWAHILI
- See more
at:
http://jamiimoja.blogspot.com/2014/12/mashine-yenye-uwezo-wa-kufikiri-kitisho.html#sthash.AVFXLpVc.dpuf
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MASHINE YENYE UWEZO WA KUFIKIRI KITISHO”
Post a Comment