Wednesday, December 3, 2014

KAMPUNI YA BIA SERENGETI BREWERIES YATANGAZA NEEMA KWA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA.


Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Serengeti breweries Bw Steven Gannon(wa katikati) akiwa na Mgeni Rasmi Bi . Quip Mbeyela ambaye alimuwakilisha  mkuu wa wilaya mbeya


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Serengeti breweries Bw Steven Gannon akizungumza na wageni waliofika katika ufunguzi wa ghala hilo.


  Kaimu Katibu tawala wilaya ya Mbeya  bi. Quip Mbeyela ambaye alimuwakilisha  mkuu wa wilaya mbeya








Gari Aina ya Scania likitoka nje tayari kwa kuanza kufanya kazi ghala hilo





Wakina dada wakiendelea kuburudika na Bia ya Kampuni ya Serengeti breweries mara baada ya ufunguzi wa ghala.


Na David Nyembe,Mbeya
Kampuni  ya Serengeti breweries Mkoani Mbeya (SBL)imetoa Rai kwa wazazi na walezi wasio na uwezo wa kuwasomesha watoto wao elimu ya juu kupeleka maombi ili waweze kupata udhamini kutoka katika kampuni hiyo.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa uhusiano wa kampuni hiyo bw. Evance Mlelwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa ghala mpya ya kuhifadhia vinywaji vinavyo zalishwa na kampuni hiyo.
Mlelwa amesema kuwa  kampuni hiyo inatoa ufadhili wa asilimia miamoja (100) na kwamba hadi sasa kampuni ya serengeti breweries imewafadhili wanafunzi zaidi ya 30.

Kuhusiana na  ujenzi huo wa ghala Mlelwa amesema ujenzi huo umeghalimu sh.500milioni ambapo ghala hilo limejengwa katika eneo la Iyunga jijini hapa.

Aidha kwa upande wake  Kaimu Katibu tawala wilaya ya Mbeya  bi. Quip Mbeyela ambaye alimuwakilisha  mkuu wa wilaya mbeya amesema serikali bado inatambua mchango mkubwa unaotolewa na kampuni hiyo hususani katika suala la ajira.

Amesema kwa kiwango kikubwa sekta binafsi ndio imekuwa mchango mkubwa kwa serikali katika suala la ajira hivyo hatua hiyo inastahili pongezi kwani imeongeza fursa za ajira kwa wakazi wa eneo hilo na jiji la mbeya kwa ujumla.
Mwisho.

0 Responses to “KAMPUNI YA BIA SERENGETI BREWERIES YATANGAZA NEEMA KWA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA.”

Post a Comment

More to Read