Tuesday, December 2, 2014

MWAKYEMBE AKABIDHI RIPOTI YA MGOGORO WA RELI




Waziri wa uchukuzi Dkt. Harison Mwakyembe  jana amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa migogoro ya shirika la reli nchini TRL, kwa lengo la kuitatua  katika shirika hilo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo na kamati iliyokuwa ikifanya uchunguzi na kuongozwa na mwenyekiti wake Mhandisi Malima Bundara, Dkt. Mwakyembe amesema, ataifanyia kazi na kuitolea maauzi jumatatu Decemba 8 mwaka huu.

Hata hivyo amesema pamoja kuwa ripoti hiyo bado hajaipitia amesomewa tu mapendekezo ya kamati na amebaini kuwepo kwa lugha laini zisizo na mwelekeo wa kuwawajibisha wale wanaosababisha migogoro ndani ya shirika.

Nae mwenyekiti wa kamati hiyo Mhandisi Malima Bundara amesema kamati imekamilisha jukumu iliyopewa, na kumkabidhi ripoti waziri, huku akibainisha baadhi ya mapendekezo ya kamati mbele ya wafanyakazi waliokuwa wakiisubiri ripoti hiyo wakiwa na imani ya kutatuliwa kero zao.

Hata hivyo baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo wamekubali kwa shingo upande huku baadhi yao wakilalamika kutopewa mishahara yao kwa muda mrefu sasa hali inayosababisha wafanyakazi hao kuishi maisha magumu.

0 Responses to “ MWAKYEMBE AKABIDHI RIPOTI YA MGOGORO WA RELI ”

Post a Comment

More to Read