Tuesday, December 16, 2014
NEWS ALERT: SIMBA YAMFUKUZISHA MAXIMO JANGWANI MARA BAADA YA KUWAPA KIPIGO CHA MAGOLI 2 KWA 0 YANGA
Do you like this story?
Na Baraka Mbolembole, Dar es
Salaam,
Baada ya kuchapwa mabao 2-0 na
mahasimu wao wa soka Simba SC katika mchezo wa ‘ Hisani Nani Mtani Jembe’ siku
ya Jumamosi iliyopita, klabu ya Yanga SC imeamua kufikia maamuzi magumu ya
kumfuta kazi kocha Marcio Maximo na ni wazi Mholanzi, Hans Van De Pluijm
atachukua nafasi hiyo. Hii ni mara ya pili kwa Yanga kumfukuza kazi kocha wao
mara baada ya kufungwa na Simba. Ikumbukwe mwaka uliopita, Mholanzi, Ernie
Brandts aliondoshwa baada ya kufungwa mabao 3-1 katika Mtani Jembe.
Tofauti na ilivyokuwa kwa Brandts
ambaye aliifundisha Yanga kwa mwaka mmoja na kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi
kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/13, Maximo yeye amefukuzwa baada ya kuiongoza
timu hiyo katika michezo tisa ndani ya miezi mitatu. Yanga imepoteza michezo
miwili kati ya saba ya ligi kuu msimu huu, Maximo ambaye alianza vizuri klabuni
hapo kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii,
alipoteza mchezo wa kwanza tu wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa
Jamhuri, Morogoro.
Yanga imeshinda michezo minne msimu
huu, lakini hadi l,igi inasimama katika raundi ya saba hakuna mtu alikuwa na
shaka kuhusu uwezo wa Maximo. Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya
Tanzania, Taifa Stars amechokwa haraka sana na mashabiki, wapenzi, wanachama na
viongozi wa klabu yake kutokana na kiwango kidogo cha uchezaji. Mifumo yake ya
ufundishaji imekosa mvuto, lakini kitendo cha kufungwa kidhaifu na Simba
kimeshindwa kuvumilika.
COUTINHO, JAJA, EMERSON WAMPONZA?
Ndiyo sababu kubwa, ukitoa mbinu zake, Maximo alikuwa akiwakumbatia zaidi
wachezaji raia wa Brazil, Andrey Coutinho, Geilson Santos ( ambaye aliomba
mwenyewe kuachwa baada ya michezo saba), kwa Emerson Oliveira siwezi
kuzungumzia kwa sababu mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo alicheza katika
kiwango cha kawaida wakati alipoichezea Yanga kwa mara ya kwanza.
Jaja alifunga mara mbili dhidi ya
Azam, ila alikosa makali katika ligi kuu kiasi cha kufunga bao moja tu katika
michezo saba ya ligi kuu. Alishindwa kumudu presha ya mashabiki wa Yanga ambao
hawakuwa wakipendezwa na kiwango chake huku uchezaji wake wa taratibu ukiwaboa
wengi. Maximo aliwanyima nafasi washambuaji kama Said Bahanunzi, Jerry Tegete,
Saimon Msuva, Hussein Javu na Hamis Kizza hata pale wachezaji hao wa Kibrazil
waliposhindwa kufanya vizuri.
Kuwang’ang’ania wachezaji hao na
kuwanyima nafasi wale wenye uwezo kumewakera . Brandts aliondolewa baada ya
kufungwa 3-1 licha ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili zaidi, yeye
aliondolewa kwa kuwa alipingana na uamuzi wa viongozi kuwasajili baadhi ya
wachezaji ambao hakuwataka wakati ule.
Brandts ndiye mwalimu aliyeifanya
Yanga kucheza mchezo mzuri wa kupasiana na ndiye aliyeimarisha kiwango cha
wachezaji kama, Saimon Msuva, Frank Domayo ( yuko Azam FC kwa sasa), Juma
Abdul, Oscar Joshua na wengineo lakini kwa Maximo imekuwa ni tofauti, wachezaji
wengi wameshuka viwango na ameshindwa kuwaimarisha wachezaji ambao ‘
wanasua-sua’. Yanga wamefanya uamuzi sahihi kwa kumuondoa Maximo na Coutinho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NEWS ALERT: SIMBA YAMFUKUZISHA MAXIMO JANGWANI MARA BAADA YA KUWAPA KIPIGO CHA MAGOLI 2 KWA 0 YANGA”
Post a Comment