Saturday, January 16, 2016

MECHI 6 AMBAZO HUTAKIWI KUZIKOSA MICHUANO YA CHAN 2016




Zimebaki saa chache kabla ya michuano ya CHAN 2016 kuanza kutimua vumbi inchini Rwanda. Nchi wenyeji watafungua michuano hiyo dhidi ya Ivory Coast kwenye dimba la Amahoro uwanja mkubwa kuliko viwanja vingine vya nchi hiyo.

Mchezo huo utakuwa ni wa kuhitaji ushindi wa lazima kwa upande wa Rwanda mechi hii itakuwa na uzito wa hali ya juu kwenye mashindano hayo.

Tuachane na mechi hiyo, sasa tuangalie mechi sita ambazo zinatarajiwa kuwa na msisimko wa hali ya juu.

6. Cameroon vs. DR Congo
Group B, 25/01/2016, 16:00hrs CAT.
Cameroon itakutana na miamba ya soka la Afrika ya kati kwenye uwanja wa Huye kwenye jimbo la Kusini mwa Rwanda. Wakongwe hao wa soka la Afrika Magharibi wakuwa wamebeba jina kubwa la nchi yao kwenye soka la Afrika lakini Congo DR inaongozwa na wachezaji wa kikosi bora cha TP Mazembe kilicho sheheni wachezaji lukuki wa ndani ya Afrika.

Mechi hiyo itawavutia wapenzi wengi wa soka ambao watasafiri kwenda DR Congo  kushuhudia pambano hilo. Itakuwa bonge la mechi.

5. Morocco vs. Rwanda
Group A, 24/01/2016, 16:00hrs CAT
Game hii itakuwa ni kama bomu kwenye michuano hii. Morocco mara zote ni timu ngumu kwa wapinzani siku zote. Ligi yao ni ngumu na aina yao ya uchezaji ni ya kimbinu. Wenyeji watakuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo huu ili kujihakikishia kufuzu kwa ajili ya hatua ya robo fainali. Hii inamaanisha mashindano yatazidi kuwa magumu na mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Amahoro unatarajiwa kuwa mgumu.

4. Tunisia vs. Nigeria
Group C, 22/01/2016, 15:00hrs CAT
Stade de Kigali ndipo pambano hili litakapopigwa kati ya miamba hiyo ya soka la Afrika. Bila ubishi mechi hii hutakiwi kuikosa kama shabiki wa kweli wa soka la Afrika.

3. Morocco vs. Ivory Coast
Group A, 20/01/2016, 18:00hrs CAT
Pambano hili la Kundi A litakuwa ni kali hasa kwenye hatua ya makundi, Morocco dhidi ya Ivory Coast ni mechi ambayo itawakutanisha pamoja miamba ya soka ya Kaskazini mwa Afrika dhidi ya wale wa Magharibi ya Afrika. Usitarajie lele mama kwenye mchezo huu siku hiyo, itakuwa ni vita isiyo na silaha. Hutakiwi kukosa kuishuhudia mechi hii.

2. Mali vs. Uganda
Group D, 19/01/2016, 18:00hrs CAT
Kwa hali ya kawaida unaweza kudhani mechi hii itakuwa ni ya kawaida sana lakini unatakiwa kufikiria kwa makini sana ni waganda wangapi watasafiri kuelekea Rwanda kushuhudia pambano hili. Uhusiano wao na Rwanda utaifanya mechi hii kushuhudiwa na mashabiki lukuki, mwisho wa siku huu utakuwa ni mchezo mkubwa siku hiyo.

1. Rwanda vs. Ivory Coast
Group A, 16/01/2016, 15:00hrs CAT
Huu ni mchezo ambao kila mnyarwanda anausubiri. Utakuwa ni mchezo muhimu si kwa timu ya taifa ya Rwanda pekee bali kwa michuano hiyo pia. Ushindi kwa Rwanda unaweza kuchagiza ushindi kwenye michezo mingine ya timu hiyo. Unatarajiwa kuwa kati ya michezo ambayo itakuwa na mashabiki wengi wengi kwenye dimba la Amahoro na hiyo inamaanisha itakuwa ni fursa nzuri kwa wachezaji na mashabiki pia.

Ivory Coasta watakuwa na wakati mgumu kwa upande wa mashabiki kawasababu wanyarwanda wanatarajiwa kuuteka uwanja huo kwa kelele za kushangilia timu yao ukizingatia ni mchezo wao wa ufunguzi kwenye michuano hiyo ya CHAN.

0 Responses to “MECHI 6 AMBAZO HUTAKIWI KUZIKOSA MICHUANO YA CHAN 2016”

Post a Comment

More to Read