Thursday, December 18, 2014

WANAJESHI 54 WA NIGERIA WAHUKUMIWA VIFO KWA KUSHINDWA KUPAMBANA NA BOKO HARAM.




Mahakama ya Kijeshi nchini Nigeria imewahukumu adhabu ya vifo wanajeshi wake 54 waliokataa kupambana na wapiganaji wa Kundi la Boko Haram.
Wanajeshi hao walikutwa na hatia ya uasi, kushambulia na uoga. Wanajeshi hao wanashutumiwa kukataa kupigana kurudisha miji mitatu iliyokuwa ikishikiliwa na Boko Haram mwezi Agosti.

Mwanasheria wa wanajeshi hao amesema wamehukumiwa vifo kwa kupigwa risasi na kikosi maalum huku wanajeshi wengine watano wakiachia.

Vikosi vya Kijeshi vya Nigeria vimedai kuzidiwa silaha na Boko Haram, kwa kuwa hawapatiwi silaha za kutosha kupambana na wanamgambo hao.

Boko Haram…



0 Responses to “WANAJESHI 54 WA NIGERIA WAHUKUMIWA VIFO KWA KUSHINDWA KUPAMBANA NA BOKO HARAM.”

Post a Comment

More to Read