Saturday, January 3, 2015
HABARI KAMILI YA CHANZO CHA PANYA ROAD KUFANYA VURUGU JANA JIJINI DAR HICHI HAPA
Do you like this story?
KIKUNDI kinachodaiwa kuwa Panya Road kimetikisa maeneo mbalimbali ya Jiji
la Dar es Salaam kwa kupora mali, kujeruhi watu na kuzua sintofahamu katika
maeneo ya jiji hilo wakiwa na mapanga mikononi.
Maeneo yaliyokumbwa
na dhooruba hiyo ni pamoja na Sinza, Tandale, Mwananyamala na maeneo mengineyo
usiku huu. Maduka na baa zimefungwa na kupelekea polisi kupiga risasi hewani
kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa kimakundimakundi.
Imeelezwa
kuwa fujo zilianzia mchana leo baada ya kiongozi wa Panya Road aitwaye Diamond
kuuawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia
mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga.
Baada ya
kumzika mwenzao leo, vijana hao wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo.
Usiku
ulipoingia wakaanza kazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Jiji la Dar.
Baadhi ya
mashuhuda walioshuhudia matukio hayo wanadai vijana hao walikuwa na silaha
mbalimbali yakiwemo mapanga na walivamia maeneo kadhaa zikiwemo baa.
Wateja
waliokuwa katika baa ya Calabash iliyopo maeneo ya Mpakani, Mwenge walilazimika
kuacha vinywaji vyao na kukimbia hovyo huku wengine wakikanyagana na kukatwa na
vipande vya chupa kwa kile kilichodaiwa kuwa vijana hao walikuwa wanakatiza
maeneo hayo japo hawakuingia ndani.
Baada ya
tukio hilo wateja wengi waliamua kurudi majumbani kutokana na baadhi yao
kujeruhiwa na vipande vya chupa wakati wakikimbia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HABARI KAMILI YA CHANZO CHA PANYA ROAD KUFANYA VURUGU JANA JIJINI DAR HICHI HAPA”
Post a Comment