Saturday, January 3, 2015

DAVID MWAMWAJA AITAMANI NDANDA FC




Kocha mkuu wa Tanzania Prisons David Mwamwaja  amesema  ana kiu ya kuchukuwa pointi tatu katika uwanja wake wa nyumbani kesho.

Akizungumza mara baada ya mazoezi katika uwanja wao wa magereza ,Mwamwaja alisema kuwa  baada ya kutoka suluhu na wagosi wa kaya Coastal Union  mechi iliyopita,sasa wamejipanga kufunguka katika mechi ya Ndanda jumapili katika uwanja wa Sokoine jijini hapa.


“Tumefanyia kazi makosa  yaliyojitokeza tulipo cheza na Coastal hasa katika safu ya umaliziaji tatizo ambalo limekuwa likiisumbua timu yangu lakini kwasasa limeisha”alisema Mwamwaja.

Timu hiyo ambayo kwasasa imeongeza mda wa mazoezi kutoka dakika 120 hadi dakika 240 ili kuendelea kujiimarisha zaidi.

Tanzania Prisons kwasasa ipo katika nafasi ya 13 kati ya timu 14 zinazo shiriki ligi kuu Tanzania Bara ambapo jumapili hii  itashuka dimbani na timu ya Ndanda Fc ya Mtwara.
Mwisho

0 Responses to “DAVID MWAMWAJA AITAMANI NDANDA FC”

Post a Comment

More to Read