Saturday, January 3, 2015

IDARA YA POLISI YAONGOZA KWA UFISADI TZ,




Jeshi la polisi nchini tanzania ndio taasisi fisadi zaidi
chini humo

Idara ya polisi ndio taasisi inayochukua hongo zaidi nchini
Tanzania kulingana na ripoti ya ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.

Ripoti hiyo inasema kuwa maafisa wa polisi walipokea
asilimia 25 ya hongo zote zilizotolewa kwa wafanyikazi wa taasisi za uma mwaka
uliopita.

Ya pili ni idara ya mahakama,ambayo wafanyikazi wake walitia
mfukoni asilimia 18 ya hongo,huku mashirika yalio na majukumu ya usajili na
utoaji wa leseni yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia 10.
kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Idara ya Polisi

nchini
Tanzania imetajwa kuwa ya tatu kwa ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Polisi wa Uganda wanaongoza wakifuatiwa na wale wa Kenya
katika nafasi ya pili na wale wa Burundi wakiwa katika nafasi ya nne.
Kulingana na ripoti hiyo maafisa wa polisi wa Rwanda ndio
wasiochukua hongo ya juu Afrika mashariki.

Utafiti huo ulifanywa mwezi Julai na Agosti mwaka uliopita
na shirika la lenye na maslahi ya kimaendeleo barani afrika ForDIA likishirikiana
na Jukwaa la uwazi nchini tanzania Trafo.

0 Responses to “IDARA YA POLISI YAONGOZA KWA UFISADI TZ,”

Post a Comment

More to Read