Tuesday, January 27, 2015

MUSWADA WA SHERIA YA USIMAMIZI WA KODI WAKWAMA




 MUSWADA wa sheria ya usimamizi wa kodi wa mwaka 2014 uliokuwa upelekwe bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura hii leo imeshindikana kutokana na idadi ndogo ya wabunge waliohudhuria.

 Kauli hiyo ilitolewa na Spika wa Bunge Anne Makinda muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge leo.

 Alisema, kwa mujibu wa ratiba shughuli ya upigaji kura ilikuwa ifanyike leo (jana) lakini kutokana na idadi ndogo ya wabunge haiwezi kufanyika.

 "Lakini muswada huu wa 'Administration ' Una kazi ndogo tu ya kupiga kura,sasa tunatambua kwamba ,wabunge wengi bado hawajafika ,na muswada huu unahitaji theluthi mbili kutkka Bara na theluthi mbili kutkka visiwani,hii haiwezi kupatikana kutokana na idadi ya wabunge ambao wameshafika Bungeni." alisema Spika Makinda

 Makinda alisema, ili wapige kura inahitajika uwepo wa theluthi mbili ya wabunge kutoka bara na thelusi mbili kutoka visiwani idadi ambayo haijafikiwa.

Mbali na muswada huo wa sheria ya usimamizi wa kodi,muswada mwingine uliokuwa uwasilishwe leo  ni muswada wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2013 ambao umeshindwa kupelekwa kutokana na serikali kuendelea kuufanyia kazi.

"Muswada wa takwimu bado Serikali inataka kuufanyia kazi ,hivyo umeondolewa kwenye miswada inayohusika." alisema

0 Responses to “MUSWADA WA SHERIA YA USIMAMIZI WA KODI WAKWAMA ”

Post a Comment

More to Read