Tuesday, January 27, 2015
TEMBO WASIO NA MENO WAONGEZEKA KATIKA MBUGA NCHINI
Do you like this story?
SERIKALI imekiri kuwa ni kweli
kuna taarifa za kuongezeka kwa tembo wasio na meno katika mbuga hapa nchini.
Kwa mujibu wa utafiti katika Hifadhi ya Taifa Mikumi kwa mwaka 2014 mwezi januari,februari,Mei na Juni ilionyesha kuwa tembo 97 wastani wa tembo 6 kwa kundi sawa na asilimia 10.21 ya tembo hawakuwa na meno.
Akijibu swali jana bungeni mjini Dodoma naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mahmoud Mgimwa alisema ,idadi hiyo ipo ndani ya wigo wa kawaida wa tembo wasio na meno katika nchi mbalimbali Afrika ambao niasilimia 2 hadi 20.
Alisema , utafiti huo ulihusisha makundi 26 yenye wastani wa tembo 59 kwa kila kundi ambapo jumla ya tembo 950 walihusika utafiti ambao ni wa awali na umeonyesha kuwa makundi ambayo yana tembo wasio na meno yanaongezeka.

Hata hivyo alisema, utafiti huo wa awali ulilenga tu katika kuthibitisha taarifa hizo na hivyo haukuwa wa kina ili kuthibitisha kuwa kuongezeka kwa tembo wasiokuwa na meno kunasababishwa na vitendo vya ujangili vinavyofanyika katika mbuga na pia haukulenga katika kutathmini ukubwa wa tatizo hilo nchi nzima na athari zake.
Baada ya uthibitisho huo wa awali Mgimwa alisema , serikali itatenga fedha kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina ili kujua sababu za kuongezeka kwa idadi ya tembo wasiokuwa na meno.
Mgimwa alikuwa akijibu swali la mbunge wa Ole Rajab Mbarouk Mohamed ( CUF) aliyetaka kujua hatua gani za kitafiti ambazo serikali imezichukua ili kujua tatizo la tembo kuzaliwa bila meno linasababishwa na nini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TEMBO WASIO NA MENO WAONGEZEKA KATIKA MBUGA NCHINI ”
Post a Comment