Tuesday, January 27, 2015

SERIKALI YATOA AGIZO ZITO KWA MANENEJA WA SHULE BINAFSI





SERIKALI imetoa agizo kwa wamiliki na mameneja wa shule zisizo za serikali kutowafukuza wanafunzi shule kwa kigezo cha kutofikia kiwango cha ufaulu walichokiweka na kuahidi kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa watakaokiuka kuanzia sasa. 

Agizo hilo lilitolewa leo Bungeni na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa wakati akijibu swali la mbunge wa Viti maaluum Conchesta Rwamlaza (Chadema)
Dk.Kawambwa alisema, Serikali inatambua tatizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wazazi,walezi na wanafunzi ambapo wametoa nyaraka kadhaa zikisisitiza kutokaririsha,kutohamisha au kumfukuza mwanafunzi kwa kigezo cha kutofikia kiwango cha ufaulu kilichowekwa na shule

 Alisema,ili kukabiliana na tatizo hilo , januari 2014 katibu mkuu wa wizara yake alimwandikia barua mwenyekiti wa umoja wa mameneja wa shule hizo kutowafukuza wanafunzi hao ingawa bado baadhi ya shule hizo zisizo za serikali zimeendelea kukaidi.

 Katika swali lake Rwamlaza aliihoji Serikali kama inafahamu kuwa shule za sekondari binafsi zinafukuza wananfunzi wasipofikia kiwango chao cha ufaulu wakiwa kidato cha tatu na hatua gani zinazochukuliwa na Serikali.

0 Responses to “ SERIKALI YATOA AGIZO ZITO KWA MANENEJA WA SHULE BINAFSI ”

Post a Comment

More to Read