Friday, January 23, 2015
RIHANNA ASHINDA KESI DHIDI YA TOPSHOP.
Do you like this story?
Rihanna ameshinda
kesi ya madai dhidi ya duka la mavzi la Topshop juu ya fulana iliyobandikwa
sura yake.
Duka
hilo liko mtaa wa maduka yenye mavazi ghali nalo limekata rufaa kutokana na
maamuzi ya kuwa kuuza fulana zenye picha hiyo bila makubaliano na mhusika ni
kosa la jinai na hakuna haki miliki iliyowekwa dhidi ya bidhaa hiyo.
Lakini
katika kile kinachoonekana kama maamuzi muhimu ilibidi yachukuliwe kuzuia
uuzwaji wa fulana hizo za kata mkono.
Wakili
wa mwanamuziki huyo nguli wa miondoko ya POP anadai kwamba picha inayoonekana
katika fulana hiyo haikuruhusiwa kutoka,na ilichukuliwa wakati nyota huyo
alikuwa akichukua picha za video huko Kaskazini mwa Ireland kwa ajili ya wimbo
wake ulioachiliwa mwaka 2011,na hivyo duka hilo la Topshop linabaki na zuio
hilo la kutokuwa na haki ya kuuza bidhaa hiyo.
Duka
hilo kubwa lilijitetea kuwa limekuwa likichapisha sura za wasanii miaka kadhaa
iliyopita katika fulana na Rihanna si wa kwanza,wapo waliotangulia kama Elvis
Presley, Jimi Hendrix na Prince.
Kutokana
na hali hiyo Geoffrey Hobbs wakili anayetetea duka hilo anadai kuwa kuwazuia
kutouza bidhaa hiyo ni matumizi mabaya ya sheria .
Bwana
Hobbs ameongeza kwamba jamii haiamini kwamba kila sura ya mtu maarufu unayoiona
katika vazi basi imepewa ruhusa na mhusika,hata hivyo Rihanna ameshafanya
biashara na kupata faida kubwa na maduka makubwa ya mavazi kama Topshop wenyewe
na mpinzani wake River Island.
Hakuishia
hapo katika kukosoa hukumu hiyo ya maahakama kuu kwamba watu maarufu hawana
mamlaka ya kuingilia kazi zao za uzalishaji na Topshop walipoamua kutumia sura
ya mwanamuziki huyo haina maana kuwa wamempitia tu lah.
Hukumu
hiyo inadaiwa ilikuwa imeangazia na kulinda hadhi na heshima ya msanii huyo
asije akaharibiwa nia yake njema katika tasnia ya mavazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RIHANNA ASHINDA KESI DHIDI YA TOPSHOP.”
Post a Comment