Wednesday, January 28, 2015
WAASI SUDANI KUSINI WAWAACHIA HURU WATOTO.
Do you like this story?
![]() |
Wanajeshi waasi wa Sudan Kusini |
Waasi nchini Sudani kusini wamewaachia huru kundi la
kwanza la watoto waliokuwa wamechukuliwa kuwa wanajeshi, kundi hilo la watoto
lililotegemewa kuachiwa wiki chache zijazo.
Shirika
la kimataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limesema Watoto mia mbili na
themanini, wengine wakiwa wadogo wa mpaka umri wa miaka 11 walikabidhiwa katika
jimbo la jonglei kwa ajili ya kukutanishwa na Familia zao. Kulikuwa na furaha
wakati watoto hao walipokutana na ndugu zao.
Umoja
wa Mataifa unasema Wanajeshi watoto takriban 12,000 waliandikishwa katika Jeshi
mwaka jana nchini Sudani kusini.
Kundi
la walioachiwa ni sehemu ya Jeshi la waasi linaloongozwa na David Yau Yau
ambaye alisaini mkataba wa amani na Serikali mwaka mmoja uliopita.
Mwakilishi
wa UNICEF Sudani Kusini, Jonathan Veitch amesema kuachiwa huru kwa kundi hilo
la watoto ni hatua ya kwanza ya matumaini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAASI SUDANI KUSINI WAWAACHIA HURU WATOTO.”
Post a Comment