Thursday, February 26, 2015
BANGI NI HALALI WASHNGTON DC.
Do you like this story?
Mji mkuu wa Marekani Washington DC umehalalisha
utumizi wa Bangi.
Hatua
hii ya Washington inafuatia ile ya jimbo la Colorado, Alaska na Washington
state ya kuhalalisha matumizi ya mihadarati kwa starehe.
Mpango
huo umekubalika na wananchi wengi katika kura ya maoni iliyopigwa Novemba mwaka
jana lakini maafisa nchini
humo
wametofautiana na wabunge wa Republican ambao ni wengi bungeni uliosababishwa
kusitisha eneo hilo kuidhinisha mbinu za kudhibiti na kutoza kodi mhadarati
huo.
Sheria
hiyo mpya itaanza kutumika kuanzia saa tano usiku wa Alhamisi na hivyo mtu
yeyote atakayekuwa akimiliki bangi kisiri atakuwa huru kuivuta bila hofu ya
kukamatwa..
Sheria
hiyo mpya hata hivyo imezua tofauti baina ya Meya wa mji huo na bunge la
Congress.
Weneyji
wa mji huo wenye umri unaozidi miaka 21 watakuwa huru kumiliki gramu 56 ya
Bangi.
Aidha
wanauwezo wa kuipanda majumbani mwao.
Hata
hivyo sheria hiyo mpya inaharamisha kuuzwa kwa bangi na ununuzi wake.
Mji
mkuu wa Washington DC - ni wilaya maalum lakini haina uhuru na hadhi sawa na
majimbo kwa hivyo kuna dhana kuwa ilikiuka kanuni ilipoamua kupiga kura ya
maoni.
Katika
Barua iliyoandikwa na wajumbe wa bunge hilo la Congress,Meya wa Washington
Muriel Bowser ameonywa kuwa sheria za jimbo zinakiukwa iwapo sheria hiyo
maarufu itaanza kutekelezwa.
Wajumbe
hao wanadai kuwa kulingana na sheria maalum iliyopitishwa na Bajeti ya taifa
Kuhalalishwa kwa bangi ni haramu.
Bi
Bowser hata hivyo anaendelea kushikilia kukutu kuwa walifwata kanuni zote
zilizowekwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BANGI NI HALALI WASHNGTON DC.”
Post a Comment