Thursday, February 26, 2015

WANAFUNZI WATUPWA JELA BAADA YA KUIGIZA IGIZO LINALOIGUSA SERIKALI.




Wanafunzi wawili Thailand wamejikuta wakiingia kwenye mikono ya Sheria kutokana tu na igizo ambalo walitunga kwa ajili ya maazimisho ya miaka 40 ya wanafunzi wa chuo hicho kupigwa na wanajeshi wa Thailand mwaka 1973 walipoandamana kudai demokrasia.

Maazimisho yao hayakuwa na heri kwa wanafunzi wawili Patiwat Saraiyaem na Porntip Mankong ambao waliandaa igizo hilo la jukwaani.

Igizo lilionekaa kukejeli uongozi wa Mfalme wa nchi hiyo, kesi ikaenda Mahakamani wakahukumiwa kwenda gerezani kwa miaka miwili na nusu kila mmoja, mchezo huo wa ‘The Wolf Bridge’ ulichezwa katika jukwaa la chuo kikuu cha Thammasat, Bangkok.

Hukumu ya wanafunzi hao ilikuwa kifungo cha miaka mitano kila mmoja lakini walipunguziwa hukumu hadi miaka miwili na nusu baada ya kukiri kosa.

0 Responses to “WANAFUNZI WATUPWA JELA BAADA YA KUIGIZA IGIZO LINALOIGUSA SERIKALI.”

Post a Comment

More to Read