Friday, February 27, 2015

PINDA: WAZAZI WENYE WATOTO WALIOKIMBIA SHULENI KWA UTORO WAKAMATWE.




Na Eckland Mwaffisi, Kyela

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ameagiza
wazazi wote ambao watoto wao wamekimbia shule
za sekondari kutokana na utoro, wakamatwe na
kufikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Bw. Pinda alitoa agizo hilo juzi katika Wilaya ya Kyela,

mkoani Mbeya, baada ya kusomewa taarifa ya Wilaya

iliyoelezea changamoto ya utoro na tatizo la mimba
kwa wanafunzi katika shule za sekondari.

Akisoma taarifa ya Wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya Bi.
Margreth Malenga, alisema changamoto waliyonayo
kwa wanafunzi wa sekondari ni tatizo la utoro
pamoja na mimba za utotoni.

Alisema baadhi ya wanafunzi walioacha shule,
wanajihuisha na biashara katika maeneo ya mipakani
ambapo tatizo la mimba linachangiwa na umaskini
wa familia pamoja na tamaa kwa wanafunzi.

Aliongeza kuwa, Wilaya imefanya jitihada
mbalimbali zilizofanikisha kuwarudisha shuleni
baadhi ya wanafunzi.

Alisema kuanzia mwaka 2011 hadi 2014, watoto
645 waliokuwa wakisoma sekondari mbalimbali
wilayani humo waliacha shule kutokana na utoro
pamoja na kupat mimba wakiwa shuleni.

Kutokana na hali hiyo, Bw. Pinda alisema Serikali
haipo tayari kuona tatizo la utoro likiendelea kuchukua
nafasi katika shule za Serikali.

''Serikali inahangaika kujenga madarasa na maabara
lakini jambo la kushangaza wanafunzi wanakimbia
masomo bila sababu za msingi.

''Mkuu wa Wilaya, tabia hii nataka ikome kuanzia
sasa, chukueni hatua kali kwa wazazi na wanume
wanaowapa mimba wanafunzi wetu,'' alisema.

Aliwataka wanafunzi kutambua kuwa, fusra ya elimu
ambayo wanipoteza itawafanya wapoteze mwelekeo
wa maisha yao kwa siku za baadaye.

Alisema takwimu za Wilaya zinaonesha kuwa,
kuanzia mwaka 2010 hadi 2014, wanafunzi 94
wa kike wameacha shule bada ya kupata
mimba wakiwa shuleni.

''Nawaomba wanafunzi wa sekondari hapa
Kyela, msikubali kuacha masomo kwa
sababu za kipuuzi,'' alisema.

Bw. Pinda yuko mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi
akikagua shughuli za maendeleo kwenye Wilaya
mbalimbali na ujenzi wa maabara.

0 Responses to “PINDA: WAZAZI WENYE WATOTO WALIOKIMBIA SHULENI KWA UTORO WAKAMATWE.”

Post a Comment

More to Read