Friday, February 27, 2015
MWENYEKITI UVCCM MKOA WA MBEYA AWAASA VIJANA KUDUMISHA AMANI
Do you like this story?
Mashabiki na wachezaji wa Timu ya Inyala wakishangilia ushindi wao mara baada ya kuiadhibu timu ya Iwalanje kwa mikwaju ya Penati . |
Mwenyekiti Kajuna akipokelewa na na wananchi wa kijiji cha Tembela kabla ya Fainali hizo kuanza. |
VIJANA mkoani Mbeya wametakiwa kutumia gharama za aina yoyote ili kulinda umoja, usalama na amani ya Mkoa pamoja na taifa kwa ujumla kwa kuepuka vitendo vinavyoweza kuashiria machafuko.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoa wa Mbeya,Amani Kajuna, alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na wachezaji katika fainali ya ligi ya mpira wa miguu ya Tarafa ya Tembela iliyofanyika jana katika kiwanja cha shule ya Msingi Iwalanje wilaya ya Mbeya.
Kajuna alisema ikiwa vijana hawatajitoa kuwa wazalendo kwa nchi yao pindi machafuko yatakapotokea watakapokimbilia mipakani mwa nchi walizopakana nazi majina yatabalidilishwa na kuitwa wakimbizi.
Alisema ili kuepuka kuitwa wakimbizi ni lazima vijana ambao ni wengi katika taifa wakajitoa kwa gharama yoyote kulinda amani na utulivu uliopo ikiwa ni pamoja na kuwaogopa wanasiasa kuwadanganya na kuwashawishi kuingia kwenye tabia hatarishi.
Aidha Kajuna alitumia muda huo kuwasihi vijana kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ikiwa ni pamoja na kuipigia kura katiba inayopendekezwa.
Awali katika mchezi huo wa fainali ambao ulizikutanisha timu za Inyala fc na Iwalanje zote kutoka Tarafa ya Tembela ambapo timu ya Inyala ilishinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6 dhidi ya penati 5 za Iwalanje fc.
Timu hizo zililazimika kupigiana mikwaju ya penati baada ya dakika tisini za muda wa kawaida kuisha kwa bila timu kushindwa kuliona lango la mwenzake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano hayo, Yohana Monga, alisema ligi ya Tarafa ilianza Januari tatu mwaka huu ikishirikisha timu 17 kutoka katika Kata tano za Tarafa ya Tembela.
Alisema ligi hiyo iliokuwa imedhaminiwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Aman Kajuna ambaye pamoja na gharama za zawadi kwa washindi alitoa jumla ya shilingi Milioni 1,250,000.
Alizitaja zawadi zilizotolewa kwa washindi kuwa ni mshindi wa kwanza ambaye ni timu ya Inyala shilingi 300,000. Mshindi wa pili ambaye ni Iwalanje shilingi 200,000, mshindi wa tatu shilingi 100,000.
Aliongeza kuwa zawadi zingine zilienda kwa mfungaji bora, mwamuzi bora, mlinga mlango bora na mchezaji bora ambao kila mmoja alijinyakulia shilingi 50,000 huku Kamati ikipewa shilingi 300,000 pamoja na mchifu wanne ambao kila mmoja alipewa shilingi 20,000/=.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MWENYEKITI UVCCM MKOA WA MBEYA AWAASA VIJANA KUDUMISHA AMANI”
Post a Comment