Wednesday, February 25, 2015

! MBWA MSTAAFU WA POLISI AAGWA KISHUJAA, AANDALIWA GWARIDE NA KUPIGIWA SALUTI NA POLISI






Mbwa mmoja wa Polisi huko New Jersey Marekani mwenye umri wa miaka nane aliyefanya kazi kwa miaka minne amelazimika kustaafu kutokana na afya yake kuwa mbaya.


Mbwa huyo wa Polisi ambaye anaitwa Judge amepewa heshima na kuagwa kishujaa, kaandaliwa na gwaride pamoja na kupigiwa saluti na Polisi tukio ambalo lilishuhudiwa pia watu wa haki za wanyama.
Judge alikuwa anastaafu kama mbwa wa Polisi huko West Deptford Township, ambapo alitakiwa kustaafu tangu mwaka 2013, kutokana na maradhi ya meno na pia afya yake ilianza kuzorota kwa kasi.

Tangu ameanza kuumwa 2013 hali ya afya yake haikuwahi kuwa nzuri, watu wa haki za wanyama waliona ni vizuri ‘astaafishwe’ na pia wakashauri aendelee kupatiwa matibabu katika Hospitali ya wanyama ya Swedesboro.



0 Responses to “! MBWA MSTAAFU WA POLISI AAGWA KISHUJAA, AANDALIWA GWARIDE NA KUPIGIWA SALUTI NA POLISI”

Post a Comment

More to Read