Wednesday, February 25, 2015

BAADA YA KUMPIGA 'STOP' BURUHANI...MBEYA CITY FC YAONGEZA DOZI.


Afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten



(Picha na Fahari News)                          

BAADA ya kumuondoa kikosini kipa namba moja, David Buruhani kwa tuhumu za kuihujumu timu katika kipigo cha 3-1 kutoka kwa Yanga mwishoni wa wiki iliyopita, Mbeya City ipo katika maandalizi makali kuiwinda Ruvu Shootings katika mechi ya ligi kuu.

City na Shootings zitachuana uwanja wa Sokoine, Mbeya, siku ya jumamosi, februari 18 mwaka huu.
Afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten ameuambia mtandao huu usiku huu kuwa timu yao inaendelea na mazoezi mara mbili kwa siku lengo likiwa ni kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa kutoka Pwani.

"Hali ni tulivu kabisa, timu imetulia, tunaendelea na mazoezi yetu vizuri. Kocha Mwambusi (Juma) anaendelea kufanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza mechi iliyopita ambayo tulicheza kwa kiwango, lakini tunahisi kulikuwa na mkono wa mtu". Amesema Dismas.

Mpaka sasa Mbeya City wapo nafasi ya 12 ya ligi kuu wakijikusanyia pointi 17 baada ya kucheza mechi 15.
Wameshinda mechi 4, wamefungwa 5 na wametoa sare 6.
Msimu uliopita, City walifungwa mechi tatu tu msimu mzima, lakini msimu huu wamevunja rekodi yao tena mapema raundi ya 15.

0 Responses to “BAADA YA KUMPIGA 'STOP' BURUHANI...MBEYA CITY FC YAONGEZA DOZI.”

Post a Comment

More to Read