Wednesday, February 25, 2015
MKUU WA MKOA WA NJOMBE ASHAURI MAVAZI YA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI KUBADILISHWA
Do you like this story?
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Njombe Kepten Mstaafu Aser Msangi akikagua wanafunzi wa shule ya msingi Ninga ambao wanatumia sare za mkaptula |
Dr Nchimbi alitoa rai hiyo leo wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha RCC na kuongeza kuwa kutokana na hali ya hewa ya baridi kali mkoa wa Njombe ni vema viongozi mkoani hapa kuangalia uwezekana na kufanya mabadiliko ya sare hizo za wanafunzi ili kuvaa suruali.
Alisema kuwa hali ya hewa ya mkoa wa Njombe ni hali ya baridi kali hivyo kuna haja ya wanafunzi hao kulinda kiafya zaidi kwa kubadilishiwa sare hizo ili kuvaa suruali kwa ajili ya kujisitili na baridi kali .
"Ndugu wajumbe mkoa wetu ni mkoa wenye baridi kali hivyo kuendelea kuwaacha watoto wetu kutumia sare hizi za kaptula ni kuwatesa zaidi ......naona si vibaya kubadili sare na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuelezwa sababu hii mbona wanaume wa Njombe kutokana na baridi hii wanavaa suruali tena wengine wanavaa mbili zaidi sasa iweje watoto wetu kuendelea kuteseka na baridi"alisema
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa alitaka viongozi wa mkoa wa Njombe kuwa na jibu moja kwa swali la ujenzi wa maabara na uhaba wa madawati kwa kila wanapoulizwa waseme wamekamilisha ujenzi huo wa maabara mbali ya kuwa wamekarabati vyumba vya madarasa yaliyokuwepo.
" Naomba tuwekane sawa hapa kuna vijimaneno maneno vimeanza kusikika kuwa hatujakamilisha ujenzi wa maabara ukweli sisi tumetumia mbinu zetu kukamilisha maabara kama tumegeuza vyumba vya madarasa hiyo ni mbinu yetu wao walitaka maabara na maabara zote zipo na sisi hatuna upungufu wa vyumba vya madarasa wala maabara "
Wakati huo huo serikali ya mkoa wa Njombe imewataka viongozi wanaohusika na migao ya fedha za uondeshaji wa mikoa kuutazama mkoa wa Njombe kwa jicho la tatu ili mgao wake uwe mkubwa zaidi kama njia ya kuuwezesha mkoa huo kusonga mbele mbele kimaendeleo.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Nchimbi alisema kimsingi mtoto ndie anayepata mahitaji bora ili apate kukua hivyo mkoa wa Njombe wenye utajiri mkubwa wa chuma na makaa ya mawe unahitaji kutengewa bajeti kubwa zaidi ili kuweza kupita hatua na kuweza kuwa mkoa wa kiuchumi kwa Taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKUU WA MKOA WA NJOMBE ASHAURI MAVAZI YA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI KUBADILISHWA ”
Post a Comment