Tuesday, February 10, 2015
MTOTO MKUBWA AZALIWA MAREKANI.
Do you like this story?
Mwanamke
mmoja nchini Marekani amejifungua mtoto mwenye uzito wa paundi 14.1 sawa na
kilo 6.4kg na sasa mtoto huyo anakula mara mbili zaidi ya uwezo wa mtoto
mchanga .
BiMaxxzandra Ford amepata mtoto aliyempa jina Avery,
ndiye mtoto mkubwa na mzito kuwahi kuzaliwa katika hospitali ya wanawake ya
mtakatifu Joseph iliyoko Tampa, Florida.Avery, alizaliwa kwa njia ya kawaida .
Ford alikuwa hajatanabahi kuwa yu mjamzito mpaka
alipotimiza wiki 35 .lakini mara baada ya kuwa anaongezeka uzito kupita kiasi
,madaktari wakamthibitishia kuwa yu mja mzito,na kutokana na kasi ya unenepaji
mwanzo Bi Ford alihisi atajifungua watoto pacha,kumbe sivyo.
Debbie Moore, mkunga katika hospitali hiyo,
wasingemruhusu mwanamke huyo ajifungue kwa njia ya kawaida kama wangegundua
mapema ana mtoto mwenye kilo nyingi kiasi hicho .
Avery anabaki hospitalini chini ya uangalizi maalumu
tangu alipozaliwa tarehe 29 January , lakini anatarajiwa kuruhusiwa kwenda
nyumbani hivi karibuni .
Bi Ford, anaye mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja
na mtoto wa kike mwenye miaka mitano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTOTO MKUBWA AZALIWA MAREKANI.”
Post a Comment