Tuesday, February 10, 2015

TAARIFA: JENGO LA MTAA WA JAMHURI NA MOSQUE JIJINI DAR LAWAKA MOTO.

Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto vikiwasili eneo la tukio mtaa Jamuhuri na moski.

Mmoja wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo hilo lililopo mtaa wa Jamuhuri na Moski-Kariakoo jijini Dar.

Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Jamuhuri na Mosque jijini Dar es salaam na kuteketeza  mali kadhaa. Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio kwa sasa kikiendelea kukusanya kila kinachojiri,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliopo eneo la tukio wanaeleza kuwa chanzo cha
moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi limefika eneo la
tukio kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo huku magari ya zimamoto
nayo yakiendelea kuwasili kupambana na moto huo..

0 Responses to “TAARIFA: JENGO LA MTAA WA JAMHURI NA MOSQUE JIJINI DAR LAWAKA MOTO. ”

Post a Comment

More to Read