Wednesday, February 25, 2015
SAKATA LA ESCROW: ANDREW CHENGE AMEKATAA KUHOJIWA NA BARAZA LA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Do you like this story?
ALIYEKUWA Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa Kamati
ya Uandishi katika Bunge Maalum la Katiba (BMK) Andrew Chenge amekataa kuhojiwa
mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma juu ya tuhuma za
kunufaika na fedha zilizotoka katika akaunti ya Tegeta Escrow, wakati
alipoitika wito katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Chenge
alitajwa kuwa mmoja wa watu waliopewa fedha na Mkurugenzi wa kampuni ya PAP,
James Rugemalila, zilizotolewa katika akaunti hiyo ya umma ambayo ilikuwa
ikihifadhi hela za Tanesco na IPTL, kiasi cha shilingi bilioni 1.6, kitendo
kilichosababisha kuondolewa katika nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya Bajeti
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lakini
baada ya kufika mbele ya kikao cha Baraza hilo, kilichokuwa chini ya Mwenyekiti
wake, Jaji Mstaafu Hamis Msumi, Chenge alisema hawezi kuhojiwa na kikao hicho
kwa vile suala lake tayari lipo mahakamani, kauli iliyomfanya Msumi na wajumbe
Selina Wambura na Hilda Gondwe kukosa la kufanya.
Baadaye
Jaji Msumi aliwaambia waandishi wa habari kuwa atatoa tamko la Baraza kuhusu
suala hilo kesho, huku likijiandaa pia kuwaita na kuwahoji wanasiasa wengine,
akiwemo Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka, ambaye naye alipewa kiasi kama hicho cha fedha.
Wengine
watakaoitwa kuhojiwa ni pamoja na mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, Mkuu wa
wilaya ya Korogwe, Mrisho Gumbo na kiongozi mwandamizi wa Ikulu, anayetajwa kwa
jina la Shaaban Gurumo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SAKATA LA ESCROW: ANDREW CHENGE AMEKATAA KUHOJIWA NA BARAZA LA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA”
Post a Comment