Wednesday, February 25, 2015
STRESS HAZIPUNGUZWI KWA KUCHEPUKA!
Do you like this story?
LABDA haijawahi kukukuta, lakini maisha
tunayoishi katika wakati wa sasa yanasababisha watu wengi wanapatwa na msongo
wa mawazo, maarufu kama stress. Hali ni mbaya kwa wafanyakazi wenye mabosi
wakorofi na hata wafanyabiashara wanaoyumba kiuchumi.
Lakini
inakuwa mbaya zaidi mambo yanapoharibika ndani ya familia, kwa maana ya
wanandoa au walio katika uhusiano wa kimapenzi. Ingawa sina takwimu kamili,
lakini uzoefu unaonyesha tafrani katika ndoa zinasababisha watu wengi sana
kuchanganyikiwa na hata kusababisha kukosa amani ndani ya mioyo yao.
Na
siyo kukosa amani na kuchanganyikiwa tu, wengi pia wamepoteza maisha baada ya
kushindwa kuhimili mikanganyiko iliyotokea. Mtu anaona mwenzake anakwenda
ndivyo sivyo katika uhusiano wake anaamua kujimaliza mwenyewe, achilia mbali
wanaoamua kujimaliza wote ili kila mmoja akose.
Ukiachana
na hawa wanaokosa uvumilivu, kuna wale ambao badala ya kufanya vitu kama hivyo,
wao huamua ‘kuchepuka’ ili kupunguza stress zinazotokana na mikwaruzo katika
familia. Yaani ili mama aondoe ‘hasira’ za baba kumzingua jana yake,
anachofanya ni kumkumbuka mtu wake wa zamani, mume wa mpangaji mwenzake
aliyemkonyeza jana, jirani yao nyumba ya pili au hata kiserengeti boy chake na
kwenda kuburudika nacho.
Anafanya
hivi kwa akili zake akiamini kuwa anajisahaulisha machungu au kama wengi
wanavyochukulia kuwa wanawakomoa wenza wao. Wachepukaji wenzao wakiwauliza vipi
kuhusu waume zao, ni rahisi kuwabeza na kuwadharau!
Hali
kadhalika akina baba nao baada ya kushindwa kuelewana na wake zao, kinachofuata
ni kuangalia katika orodha ya walio katika simu na kumkumbuka Mwajuma Ndala
Moja, jirani anayejigonga kila siku, mfanyakazi mwenzake ofisini au hata dada
wa dukani anayemchekeaga akienda kupata mahitaji.
Akienda
huko, hata anaochepuka nao wanapojaribu kujifanya kumuogopa mkewe au rafiki
yake, ni rahisi kukutana na majibu kama haya; “achana naye mjinga huyo, wewe
tulia kula maisha” au “Anajifanya anajua wakati anaungua na jua, achana naye.”
Lakini
unapojaribu kuangalia suala hili, unajikuta unagundua kwamba hakuna yeyote kati
yao ambaye kwa kweli anaondoa stress zaidi ya kuongeza matatizo. Utakwenda nje,
sawa, lakini kumbuka huendi kule baada ya kumbusu na kumdanganya mwenzio, bali
unakwenda ukiwa umenuna na hutaki hata kuaga unakoenda.
Matokeo
ya uchepukaji wa namna hii ni kukosa uangalifu na umakini katika ufanyaji wa
tendo, kitu ambacho kinaweza kuleta athari, siyo tu kwa mhusika, bali hata kwa
mtu wake aliyemuacha nyumbani.
Ukiachana na athari za kiafya kwa mfano, lakini hata lugha ya dharau kwa mwenza wako unayoitoa, nayo inaweza kuleta madhara kwa upande wa pili kwa sababu tayari watu wa nje wanatambua udhaifu uliopo ndani mwenu. Yule jirani uliyechepuka naye atatangaza kwa marafiki zake juu ya ugomvi wenu na jinsi ulivyomdharau mume au mke wako.
Hiyo
itasaidia kuzidi kumdharaulisha mume au mke wako mtaani kwenu kwa sababu watu
watamuona mwenzako kama mtu rahisi na asiye na maana. Kitu cha msingi
unachopaswa kufanya kila inapotokea kutoelewana ndani ya nyumba au uhusiano
wenu, unatakiwa kuwa mtulivu kiakili kuliko wakati mwingine wowote.
Kumbuka,
huu ni wakati unaoweza kufanya kosa linaloonekana dogo, lakini likakupa madhara
makubwa. Unapohitaji kupata muda wa kujiuliza, basi usiweke mambo ya ngono
akilini mwako. Tafuta mtu unayemuamini na kumwelewa, mshirikishe tatizo lako.
Faida ya kumshirikisha mwingine katika tatizo lako ni zuri kwa kuwa mawazo
mawili matatu tofauti kutoka vichwa tofauti yatakupa mwanga wa kujua nini cha
kufanya ili kukabiliana na kilicho mbele yako.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “STRESS HAZIPUNGUZWI KWA KUCHEPUKA!”
Post a Comment