Saturday, February 28, 2015
WANAWAKE WA KIMASAI WAENDELEA KULALA PORINI BAADA YA WAUME KUKIMBIA MAKAZI YAO.
Do you like this story?
Wanawake wa Kimasai katika kijiji cha
Mabwegere wilayani Kilosa mkoani Morogoro wamelalamikia kuishi maisha magumu
baada ya wanaume kukimbia makazi na kuwaachia mzigo wa kulea familia
kufuatia mapigano yaliosababisha mauaji ambapo wanawake wengine
wamelalamikia kujifungulia majumbani kutokana na kushindwa kumudu gharama za
kwenda katika vituo vya afya.
Baadhi ya nyumba zimefungwa ambapo
wakizungumza wakiwa maporini wanawake hao wamesema baadhi ya watu wameyakimbia
makazi yao kutokana na kuishi kwa hofu ambapo wamesema migogoro hiyo ya ardhi
inawaathiri wanawake na watoto zaidi kwani wanaume wamekimbia na kuwaachia
mzigo wa kulea familia huku wengine wakikosa msaada na wengine wakishindwa
kumudu gharama za matibabu na hivyo kuomba serikali kusimamia kumaliza migogoro
hiyo.
Nae mwenyekiti wa kijiji cha Mabwegere
Mika Kashu amekiri baadhi ya wanawake kuishi katika mazingira magumu ambapo
amesema waliohusika na mauaji hayo wanafahamika na hivyo kuomba serikali
iwachukulie hatua kwani oparation ya kamatama imesababisha hofu na wanaume
kulazimika kukimbia kijiji.
Afisa utawala wa wilaya ya Kilosa
Hilary Sagala akizungumza kwa njia ya simu amesema jeshi la polisi limeimarisha
ulinzi katika eneo la Mabwegere na kuhusu wafugaji kukimbia makazi amesema
hakuna sababu ya watu kukimbia makazi kama hawakuhusika na tukio la
lililosababisha mauaji na kuwataka wananchi kurejea katika makazi yao
waendelee na shughulizao kama kawaida.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAWAKE WA KIMASAI WAENDELEA KULALA PORINI BAADA YA WAUME KUKIMBIA MAKAZI YAO.”
Post a Comment