Friday, February 20, 2015
YANGA TAMU HIYO!, MAMBO YA MSUVA USIPIME...WAPAA KILELENI WAKIIZIDI AZAM HATA WASTANI WA MAGOLI
Do you like this story?
Mchezaji wa Yanga Mrisho Ngassa akijaribu kuuwahi Mpila |
Mchezaji wa Yanga Saimon Msuva (dakika ya 3, 62’aliwanyanyua mashabiki mara baada ya kuitandika Tz Prisons |
Andrey Coutinho.(Picha zote na Fahari News) |
YANGA
SC imeitungua Tanzania Prisons mabao 3-0 katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania
bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa CCM Sokoine, Mbeya.
Mabao
ya Yanga yamefungwa na Saimon Msuva (dakika ya 3, 62’ na Andrey Coutinho 11’).
Kwa
matokeo hayo, Yanga wameishusha Azam kileleni baada ya kufikisha pointi 28
katika mechi 14 walizocheza na wanawaacha Azam nafasi ya pili wakiwa na pointi
26 kwa mechi 14 walizocheza baada ya jioni hii kutoka suluhu (0-0) na
Ruvu Shootings uwanja wa mabatini, Pwani.
Licha
ya kuwazidi Azam kwa pointi, Yanga pia wamewazidi wanalambalamba wastani wa
mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam
wamefunga magoli 22 na kufungwa 12, tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni
10, wakati Yanga wao wamefunga magoli 18 na kufungwa 7, tofauti ni 11.
Ushindi
wa leo ni salamu tosha kwa Mbeya City fc ambao watachuana na Yanga katika
uwanja wa Sokoine, jumapili ya wiki hii.
Tanzania
Prisons wameendelea kuburuza mkia wakijikusanyia pointi 11 tu katika mechi 14
walizoshuka dimbani.
Mapema
dakika ya 3’ Saimon Happygod Msuva aliifungia Yanga bao la kuongoza akimalizia
mpira wa kona uliochongwa na kiungo mshambuliaji raia wa Brazil, Andrey
Coutinho.
Msuva
aliruka juu sambamba na kipa na mpira ulipotua aliugusa kwa mbali na
ukamponyoka mlinda mlango na kuzama goli.
Wachezaji
wa Prisons walihamaki wakiamini Msuva amemsukuma kipa, lakini mwamuzi akahesabu
bao.
Bao
la pili lilifungwa dakika ya 11’ ya kipindi cha kwanza ambapo Coutinho alipiga
shuti la kawaida, beki wa Prisons akiwa katika harakati za kuokoa alijifunga
mwenyewe.
Yanga
waliendelea kucheza vizuri, wakigongeana pasi na kufika eneo la hatari la
Prisons, lakini safu ya Prisons ilifanya vizuri licha ya kupata misukosuko.
Katika
kipindi hicho, Prisons walitulia baada ya kufungwa na kupata nafasi kadhaa,
lakini walishindwa kuzitumia.
Mpaka
dakika 45’ za kipindi cha kwanza zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa mabao
2-0.
Kipindi
cha pili, Prisons walianza kutafuta mabao ya kuzawazisha, lakini Yanga
waliendelea kuonesha uzoefu wao wakiwatuliza vizuri.
Katika
dakika ya 62’ Andrey Coutinho aliingiza kona maridadi na Msuva akapiga kichwa
‘ndosi’ na kuzamisha goli la tatu.
Msuva
alipata upenyo huo kutokana na uzembe wa beki wa Prisons, Salum Kimenya
aliyekuwa anamuangalia tu wakati akimtoka kupiga kichwa.
Coutinho
leo hii amefunga goli na kusababisha magoli mawili ya Msuva kutokana na mipira
yake ya kona.
Msuva
amefikisha mabao 6 msimu huu, magoli mawili nyuma ya kinara wa kupachika mabao,
mshambuliaji wa Azam fc, Didier Fortune Kavumbagu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “YANGA TAMU HIYO!, MAMBO YA MSUVA USIPIME...WAPAA KILELENI WAKIIZIDI AZAM HATA WASTANI WA MAGOLI ”
Post a Comment