Tuesday, March 24, 2015
ANGALIA MVUA ILIVYOONDOA ROHO ZA WATU WATANO JIJINI DAR.
Do you like this story?
Watu watano
wamefariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam,
watatu kati yao wakiwamo wanafunzi wawili, wakipoteza maisha baada ya kibanda
walichojihifadhi kujikinga na mvua kuangukiwa na nguzo ya umeme na kuwaunguza.
Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoa wa kipolisi wa Temeke, Zakaria Sebastian alisema vifo
vya watu hao watatu vilitokea katika eneo la Mchikichini Kimbangulile, Mbagala.
Sebastian aliwataja
waliokufa kuwa ni Ramadhan Said (10),
mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Mchikichini, Alhaji
Jumanne (15),
mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya Charambe na Monica
Elistone (26).
Alisema wakati mvua
ikiendelea kunyesha, watu hao walijihifadhi kwenye kibanda kilichotengenezwa
kwa mabati na ghafla waya wa nguzo hiyo ulikatika na kuangukia kibanda hicho na
kushika moto.
“Wakiwa kwenye banda hilo, ghafla nguzo ilianguka na waya wake
kuangukia kibanda kilichoshika moto na kuwateketeza watu hao,” Sebastian.
Mjumbe wa shina namba
nne wa mtaa huo, Kondo Namna alisema zaidi ya nguzo saba zimeinamia
kwenye nyumba za watu na wameshatoa taarifa Tanesco, lakini hadi jana, hakuna
hatua zozote zilizochukuliwa na shirika hilo.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema wakati
mvua zinaendelea kunyesha saa sita usiku wa kuamkia jana, mkazi wa Mwananyamala
Edward Warioba (22) alifariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta akiwa amelala
nyumbani kwake.
Katika tukio jingine,
Kamanda Wambura alisema maiti ya mwanamume mwenye umri wa kati ya miaka 45 na
50 iliokotwa ikielea kwenye makutano ya Mto Goba na Makongo.
Alisema huenda mtu
huyo alisombwa na maji ya mvua katika eneo ambalo bado halijajulikana. Wakati
maafa hayo yakitokea, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imetoa tahadhari ya kuwapo kwa mvua
kubwa katika maeneo ya ukanda wa Pwani na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuwa
makini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ANGALIA MVUA ILIVYOONDOA ROHO ZA WATU WATANO JIJINI DAR.”
Post a Comment