Tuesday, March 24, 2015
ZAIDI YA WANAFUNZI 200 WA SHULE YA MSINGI KINGOLWIRA WAGUNDULIKA KUWA NA MAGONJWA WA MENONA FIZI.
Do you like this story?
Zaidi ya wanafunzi
200 wa shule ya msingi KINGOLWIRA katika manispaa ya morogoro
wamegundulika kuwa na matatizo ya kinywa na meno na baada ya madaktari wa
afya ya kinywa katika hospitali ya mkoa wamorogoro kufanya uchunguzi na
kuwasafisha meno wanafunzi.
Akizungumza wakati wa
zoezi la utoaji wa huduma ya afya ya kinywa na meno katika shule ya msingi
KIGOLWIRA na katika kituo cha kulea wazee wasiojiweza cha fungafunga mjini
morogoro Daktari wa meno Samson Tarimo amesema baada ya kufanya uchunguzi
na kuwasafisha meno wamebaini idadi kubwa ya wanafunzi meno yao yameoza
ambapo amewataka wazazi kuwapeleka watoto hospitali kw amatibabu zaidi.
Kwa upande wao baadhi
ya wanafunzi na wazee waliopata huduma hiyo wameshukuru madaktari ambapo
wameeleza walikuwa wakisumbuliwa na tatizo la meno kwa muda mrefu
bila kupata ufumbuzina kuiomba serikali kuwezesha juhudi zilizoanzishwa
na madaktari hao kuwa endelevu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ZAIDI YA WANAFUNZI 200 WA SHULE YA MSINGI KINGOLWIRA WAGUNDULIKA KUWA NA MAGONJWA WA MENONA FIZI.”
Post a Comment