Tuesday, March 3, 2015
SIMBA YAMFAIDI REFA MECHI YAO NA YANGA.
Do you like this story?
MWAMUZI
ambaye Yanga wana bifu naye, Martin Saanya amekabidhiwa kuchezesha mechi ya
watani wa jadi Jumapili ijayo, Mwanaspoti limethibitisha. Mwamuzi huyo mwaka
2009 alikuwa wa akiba wakati Yanga ilipotoka sare na Simba lakini mwaka 2013
Simba ilipolala mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa ndiye aliyechezesha.
Hata
hivyo, aliingia kwenye mzozo na Yanga baada ya kutoa penalti kwa Coastal Union
kwenye dakika za lala salama na mechi kumalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye
msimu wa 2012/13, jambo ambalo liliifanya Yanga kumchukia na kukosa imani naye.
Saanya
ambaye alifungiwa na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) mwaka mzima kwa
kushindwa kumudu mechi hiyo ambayo ilisababisha mashabiki wa Yanga kuharibu
mali za Uwanja wa Mkwakwani pamoja na basi la Coastal Union.
Kabla
ya mchezo huo, mwamuzi huyo alikuwa akituhumiwa na mashabiki wa Yanga kwamba aliibeba
Simba kwenye mechi ya hisani dhidi ya Azam. Simba ilishinda mabao 3-2 huku Azam
wakidai kunyimwa penalti mbili za wazi.
Habari
kutoka ndani ya TFF zimedai kuwa mwamuzi huyo mwenye beji ya Shirikisho la Soka
la Kimataifa (Fifa), ndiye atakayeamua nani mbabe katika mechi hiyo ambayo
itashuhudia Kocha Mserbia, Goran Kopunovic akiiongoza Simba kwa mara ya kwanza
kwenye mechi ya watani wa jadi nchini.
Tayari
Simba wametimka Jiji la Dar es Salaam na kwenda visiwani Unguja ambako mara
nyingi wanaamini wakitokea huko hupata matokeo mazuri kutokana na utulivu wa
mazingira ambao unawafanya akili zao zitulie katika jambo moja tu.
Saanya
amewahi kuichezesha mechi ya Simba na Yanga mara moja msimu wa 20012/13 kabla
ya kufungiwa na matokeo ya mechi hiyo ilikuwa ni sare ya bao 1-1. Simba
ilianza vibaya ligi hiyo na ilijikongoja na kupanda mpaka nafasi ya nne kwenye
msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 na itaingia uwanjani ikitoka kuifunga
Prisons mabao 5-0 wakati Yanga yenyewe inaongoza ligi ikiwa na pointi 31 na tayari
imefuzu hatua ya pili kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa
BDF XI ya Botswana na sasa itakutana na Platinum ya nchini Zimbabwe.
CHANZO> MWANASPOTI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMBA YAMFAIDI REFA MECHI YAO NA YANGA.”
Post a Comment