Thursday, May 21, 2015
TUME YA HAKI ZA BINADAMU YATOA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA TUHUMA DHIDI YA JESHI LA POLISI.
Do you like this story?
Na PIUS YALULA - MAELEZO
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
imelaani vitendo vya uzalilishaji vilivyofanywa kwa Viongozi wa Chama cha
Wananchi (CUF) Januari 27 mwaka huu (2015) wakati wa maandamano ya Chama hicho
Mtoni Mtongani Wilaya ya Temeke.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nanduga,
alisema uchunguzi wa tukio hilo umekamilika kwa kuzingatia kifungu cha
130[1][c],[f] na [g] cha katiba ya jamhuri ya Aidha aliongeza kuwa sheria
nyingine zilizotumika kuchunguza tukio hilo ni pamoja na kifungu cha 6[1][c]na
[g] vifungu 15[1][a] na 28[1][a],[b] na f vya Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora Na.7 ya mwaka 2001, sheria ya polisi na polisi wasaidizi, sura
322, na sheria ya vyama vya siasa, sura 258.
Nyanduga alisema Tume yake imebaini ukikwaji
mkubwa wa haki za binadamu waliofanyiwa viongozi na wanachama chama cha
wananchi CUF katika maandamano yao ya shughuli za kichama, hivyo Tume ilibaini
kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kupita kiasi, ukiukwaji wa misingi ya
utawala bora na udhalilishaji wa wanachama wawili wa kike wa CUF.
"Tume imetoa mapendekezo kwa jeshi la
polisi kuzingatia kanuni, sheria, haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika
utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku na kuhakikisha maafisa wake
wanajipanga vyema katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa operesheni
zake" alisema Nyanduga
Kwa mujibu wa Nyanduga tume hiyo pia
imewataka Viongozi na wanachama wa CUF kutafuta namna ya kuboresha mahusiano na
jeshi la polisi, ili kuondoa mivutano isiyo na tija.Tume imepanga kuitisha
mafunzo na mikutano mbalimbali kwa kushirikiana na vyama vya siasa,Tume ya
Taifa ya Uchaguzi [NEC], pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi
la Polisi na Magereza, msajili wa vyama vya siasa, na asasi za kiraia ili
kupanga taratibu zote katika kujua haki za binadamu na utawala bora
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TUME YA HAKI ZA BINADAMU YATOA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA TUHUMA DHIDI YA JESHI LA POLISI.”
Post a Comment