Wednesday, June 24, 2015
ARUSHA WAFANYA MAANDAMANO KUPINGA BVR, POLISI WAWASHIKISHA ADABU.
Do you like this story?
Polisi
mjini hapa wameyasambaratisha maandamano ya watu wasiofahamika waliokuwa na
mabango ya kutaka muda wa uandikishwaji wa wapigakura kuongezwa.
Watu
hao, ambao polisi iliwaita ‘wahuni’, waliandamana saa tatu asubuhi kwenye
Barabara ya Sokoine.
Haikuweza
kufahamika mara moja watu hao walitoka wapi, kwani wenyeviti wa mitaa ya kata
zote hawakuweza kuwatambua.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema
walilazimika kutumia nguvu kuvunja maandamano hayo kwa vile hayakuwa halali.
Sabas
alisema watu hao ni kundi la wahuni lililozuka kutaka kusitishwa uandikishaji
wa wapigakura.
Diwani
wa Kata ya Sombetini, Ally Bananga alisema hakuwa na taarifa na maandamano
hayo, lakini hashangai kutokea kwake.
“Sitashangaa watu kuandamana, kwani wamechoshwa na tabia ya
watendaji kuwarudisha nyumbani. Watu wanafika asubuhi kituoni wanaambiwa warudi
nyumbani kwa sababu hawakuandikisha majina yao,” alisema Bananga.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa JR, Jackson
Mollel aliitaka tume kutoa mwongozo
wa kuwasaidia wananchi kujiandikisha sehemu husika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ARUSHA WAFANYA MAANDAMANO KUPINGA BVR, POLISI WAWASHIKISHA ADABU.”
Post a Comment