Wednesday, June 3, 2015
MAAFISA WA MAREKANI KUMCHUNGUZA BLATTER.
Do you like this story?
Imeripotiwa kuwa Raisi wa Fifa,Sepp Blatter
anafanyiwa uchunguzi na maafisa wa marekani ili kuthibitisha tuhuma za rushwa
zinazomkabili vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.
Taarifa hiyo inakuja baada ya Blatter
kutangaza kuwa atajiuzulu wadhifa wake.
Wakati ambao waendesha mashtaka nchini
Marekani wanaoifuatilia tuhuma za rushwa walikamata maafisa saba wa Fifa nchini
Switzerland kati ya watu 14 wanaotuhumiwa kwenye kashfa hiyo.
Hata hivyo Blatter alisema anatumia mamlaka
aliyopewa hata kama hayakubaliwi na kila mtu duniani.
Fifa inahitaji mabadiliko makubwa ili kukemea
rushwa.
Mwandishi wa BBC,Nick Bryant mjini New York
anasema kuwa bado maafisa hao wa marekani wana matumaini ya kupata ushirikiano
kutoka kwenye takwimu za Fifa kwa sasa ili kubaini namna ambavyo mzunguko wa
pesa chafu unavyomuhusisha Blatter.
Katika taarifa iliyoripotiwa kutoka kwa
maafisa wa Marekani wiki iliyopita kuhusu rushwa katika shirikisho hilo la soka
ulimwenguni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Loretta Lynch haikumshutumu Blatter
moja kwa moja .
Ingawa alisema kuwa huu ni mwanzo tu wa
uchunguzi na si mwisho.
Mwandishi wetu anasema huu ni msingi wa
maafisa wa marekani katika kuikomboa dunia katika majanga makubwa kama haya.
Mwanzoni FBI,mamlaka ya ndani ya huduma za
Mapato nchini Marekani na mwanasheria wa New York , ambaye alishiriki katika
uchunguzi huo walisema kuwa hawana maoni juu ya kujiuzulu kwa Blatter.CHANZO:BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAAFISA WA MAREKANI KUMCHUNGUZA BLATTER.”
Post a Comment