Monday, June 15, 2015
SITTA:NILIWAHI KUKATAA RUSHWA YA SH 140 MILION.
Do you like this story?
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta
|
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema
anasimama kifua mbele kupambana na rushwa kwa kuwa aliwahi kuikataa rushwa ya
Dola 70,000 (sawa na Sh140,000) milioni).
Sitta alisema hayo jana wakati akizungumza na
makada wa chama hicho waliojitokeza kumdhamini katika wilaya ya Geita mkoani
Geita na kusema kuna baadhi ya watia nia wanaopita wakisema kuwa wakiwa marais
watapambana na rushwa wakati ukiwatazama macho yao yanaonyesha ni wala rushwa.
Viwango vya kubadili fedha za kigeni, kwa sasa Dola moja ya Marekani sawa na
Sh2,000.
“Nilitumwa Canada kutafuta ndege tatu, jioni
moja tukiwa Canada tunajiandaa kuondoka, akaja mkurugenzi wa masoko wa kampuni
tuliyonunua ndege, akaniambia waziri tuna kautaratibu hapa ukifanikisha ndege
zetu zikanunuliwa tunatoa bakshishi ya Dola 70,000 utataka hizi hela tuzipeleke
benki gani,” alisema Sitta akimnukuu ofisa huyo wa masoko.(P.T)
“Watazameni hawa watu... mtu kawa waziri
mwaka mmoja leo anataka urais, halafu anasema atapambana na rushwa...utapambana
na rushwa wapi wakati hata hujapita kwenye mitego ya rushwa. Watazameni kwa
makini, mtawajua tu kwa macho, kwani macho yao yamekaa kijanjajanja kweli,”
alisema. Aliendelea, “Kwa kuwa mimi nililelewa vizuri nilijua tu huo ni mtego
wa shetani, nikamwambia mkurugenzi nitampa jibu kesho, nikawasiliana na wakubwa
zangu kwanza wakakubali ni chukue hiyo pesa ikasomeshe marubani wa ndege.”
Sitta aliwataka wananchi hao kuwatazama kwa
makini watangaza nia hao, na kuwauliza iwapo tayari walishawahi kupambanishwa
na rushwa.
Lowassa aonya kuhusu viongozi wanafiki
Kigoma. Wakazi wa Kigoma wametakiwa kuwa
makini na kauli za baadhi ya viongozi wa Serikali wanaojinadi kwa kusema
wanawapenda Watanzania maskini, lakini mioyoni mwao hawana huruma.
Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu,
Edward Lowassa alipokuwa akitafuta wadhamini
mkoani hapa, muda mfupi baada ya kukabidhiwa
fomu zenye majina ya wanachama waliojitokeza kumdhamini.
Akiwa katika ofisi ya CCM mkoa, Katibu wa CCM
Wilaya ya Kigoma Mjini, Nohoji Kubaji alimkabidhi Lowassa fomu 45 za wana CCM
waliomdhamini.
“Wapo viongozi, wanajifanya wanawapenda na
kuwajali watu masikini, lakini wao wenyewe unawakuta ni matajiri, hawa jamaa ni
waongo sana hawa,” alisema.
Lowassa aliwataka wakazi Kigoma kumuombea ili
dua na sala zao ziweze kumsaidia afikie malengo aliyojiwekea. “Nina dhamira ya
kuwatumikia, lakini lazima mniombee sana dua na sala ili mambo yangu yaende
vizuri hatimaye nishinde kuwa Rais wa Tanzania. Mimi nachukia sana umaskini,
kwa hiyo lazima tuwe kama Malaysia ambayo kiongozi wake alipambana kuhakikisha
wananchi wanaondokana na umaskini,” alisema.
Wasira awashangaa wanaotumia matarumbeta
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Stephen Wasira amesema anashangazwa na baadhi ya wagombea wenzake, wanaokwenda
kutafuta wadhamini kwa matarumbeta na miziki ya kuwaita wananchi.
Wasira alitoa kauli hiyo mjini Musoma katika
Ofisi ya CCM Mkoa, Adamu Ngalawa wakati alipokuwa akipokea majina na kadi za
wadhamini waliojitokeza kumdhamini.
Alisema wagombea wanaofanya hivyo wanakiuka
taratibu, kanuni, sheria na katiba za chama kwa kuwa chama hicho tawala
kilishapitisha kuwa wakati wa kutafuta wadhamini hakuna mgomWbea kuhutubia
mkutano wa hadhara.
“Kuna wagombea wanaitisha mkutano wa hadhara
na kuwaita wananchi wakati hawana cha kuwahutubia kwa kuwa wamezuiliwa kufanya
hivyo...wanabaki wakiwaeleza wananchi mniombee, wawaombee nini? Mimi
nimeshatembea mikoa zaidi ya 20 na hakuna sehemu nimewaita wananchi tofauti na
kutoa taarifa kwenye chama ili wadhamini niwapate,” alisema.
Wasira alisema mkoa wa Mara una wagombea
wanne wanaowania urais, lakini hakuna atakayejitoa kwa misingi ya kuachiana
kura kwa sababu hakuna mwananchi wa kawaida atakayepiga kura bali maamuzi
yatafanywa na Kamati Kuu ya CCM.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SITTA:NILIWAHI KUKATAA RUSHWA YA SH 140 MILION.”
Post a Comment