Sunday, June 14, 2015
ICC YAITAKA A. KUSINI KUMKAMATA BASHIR.
Do you like this story?
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita
ICC imeitaka Afrika Kusini kumkamata rais wa Sudan Omar Al-Bashir ambaye
anaripotiwa kusafiri kwenda nchini humo kuhudhuria mkutano wa Muungano wa nchi
za Afrika ambao unaanza leo Jumapili.
Kwenye taarifa yake , ICC ilisema kuwa
waranti mbili za kumkamata Bashir bado ziko. Anatafutwa na mahakama ya uhalifu
wa kivita kuhusiana na uhalifu ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa
na kesi inayohusiana na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.
Kama mwanachama cha ICC, Afrika Kusini
inastahli kumkamata Bashir ikiwa atasafiri kwenda nchin humo . Lakini Muungano
wa Afrika umekataa kushirikiana na mahakama hiyo ya kimataifa ukisema kuwa ICC
inawaonea viongozi wa Afrika.BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ICC YAITAKA A. KUSINI KUMKAMATA BASHIR.”
Post a Comment