Thursday, June 18, 2015
TAARIFA NYINGINE MPYA KUTOKA FIFA KUHUSU RUSHWA.
Do you like this story?
Rais wa FIFA wakati akitangaza mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 . |
Wapelelezi
wanaofatilia kashfa ya rushwa inayohusu shirikisho la soka ulimwenguni FIFA
wameahidi kufichua makubwa zaidi baada ya kugundua siri nzito zilizojificha
kwenye mchakato wa kuchagua mwenyeji wa kombe la dunia.
Wapepelezi
hao wakiongozwa na Mwanasheria mkuu wa Uswisi, Michael Lauberwamesema kuwa kuna matukio karibu 53 ya uchakachuzi na utakatishaji
haramu wa fedha ambayo yamegundulika kwenye michakato tofauti ya kumpata
mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia na matukio haya yamehusishaa watu wazito
ambao kama yatagundulika undani wake yatazua hofu na utata mkubwa.
Mwanasheria
huyo ameonya kuwa hatajali kama upelelezi wake utasababisha hasara ya
fedha au kupokonywa uwenyeji kwa nchi za Urusi na Qatar na anachojali ni
ufanisi wa kazi yake na si kitu kingine.
Imedaiwa
kuwa upelelezi huu unahusisha kuhojiwa kwa viongozi wa juu wa FIFA akiwemo rais
wa zamani Sepp
Blatter ambaye hivi karibuni
alitangaza kujiuzulu siku chache baada ya kuchaguliwa kwa kipindi cha tano.
Viongozi
kadhaa wa zamani wa FIFA wakiwemo Mmarekani, Chuck Blazer na rais wa zamani wa chama
cha soka cha Trinidad and Tobago, Jack
Warner wameahidi kutoa ushirikiano kwa
wapelelezi huku wakiahidi kuwa watazungumza bila kuficha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA NYINGINE MPYA KUTOKA FIFA KUHUSU RUSHWA.”
Post a Comment