Wednesday, June 24, 2015
WAKAGUZI WA MALORI NA MABASI WATAKIWA KURUDI DARASANI ILIKUONGEZA UJUZI,MOROGORO.
Do you like this story?
Kufuatia kuongezeka kwa matukio ya ajali za barabarani jeshi
la polisi kikosi cha usalama barabani nchini wamelazika kuwarudisha darasani
askari wa kikosi cha usalama barabarani na kuwapa mafunzo ya ukaguzi wa malori
na mabasi kwa vitendo katika chuo cha mafunzo ya ufundi veta ili kuwajengea
uwezo wa kudhibiti ajali barabarani.
Wakizungumza mkoani Morogoro askari wa ukaguzi wa malori na
mabasi wamesema kufuatia kukua kwa sayansi na teknolojia ya vyombo vya
usafirishaji serikali kupitia jeshi la polisi inatakiwa kutoa mafunzo ya mara
kwa mara kwa maafisa na wakaguzi wa magari ili askari wake waweze kukabiliana
na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ongezeko la ajali za barabarani.
Kaimu mkurugenzi wa mafunzo veta kanda ya mashariki
Asanterabi Kanza akizungumza na wakaguzi hao wa malori na mabasi katika chuo
cha elimu na mafunzo ya ufundistadi veta Kihonda mkoani Morogoro amesema idadi
kubwa ya watanzani wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani
ambazo baadhi yake zinasababishwa na wakaguzi kutokuwa na utaalamu wa kutosha
kukagua magari ambapo amewataka wazingatie mafunzo ili kukabiliana na ajali
zisizo la lazima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAKAGUZI WA MALORI NA MABASI WATAKIWA KURUDI DARASANI ILIKUONGEZA UJUZI,MOROGORO.”
Post a Comment