Monday, June 22, 2015
YANGA YAMGOMEA KOCHA WAKE KUINOA STARS.
Do you like this story?
Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Charles Boniface Mkwassa. |
Na Phillip Nkini
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) imewekewa ngumu na Klabu ya Yanga, baada ya Wanajangwani hao kumgomea
kocha wao kuifundisha Taifa Stars.
Juzi
kamati hiyo ilimtimua aliyekuwa Kocha Mkuu wa Stars, Mart Nooij, baada ya
kulala kwa mabao 3-0 kutoka kwa timu ya taifa ya Uganda kwenye mchezo wa kufuzu
Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan) uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan
mjini Zanzibar.
Mara
baada ya mchezo huo, kamati hiyo ilikubaliana kumpa timu hiyo mzalendo Charles
Boniface Mkwassa, ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga na aliyewahi kuwa kocha wa
timu ya taifa ya Zanzibar, Hemed Morocco, lakini Yanga wamemgomea kocha wao
kuifundisha Stars.
Chanzo
cha ndani kimelieleza Championi
Jumatatu kuwa mara baada ya Mkwasa kupigiwa simu na kupewa dili hilo,
aliomba kuzungumza na waajiri wake wa sasa, lakini baadaye alirudisha jibu kuwa
wamemkatalia wakidai kama ni fedha watamuongezea.
“Aliomba
kuzungumza na waajiri wake ambao ni Yanga, lakini waligoma, hata viongozi wa
kamati ya utendaji waliwasiliana na viongozi wa Yanga, lakini wakaweka ngumu
kumuachia kocha huyo.
“Kwa
Tanzania kwa sasa tunaona huyu ndiye kocha anayeweza kuisaidia timu hii ikafika
mbali, unajua huyu ana leseni A ya Caf, Morocco naye ana leseni A, kwa hiyo ni
makocha wasomi.
“Bado
hatujakata tamaa, tunaamini wanaweza kukubali ingawa hali inaonekana kuwa
ngumu.
“Morocco
yeye hana shida atatua Dar es Salaam kesho (leo) kwa ajili ya kuanza majukumu
yake,” kilisema chanzo hicho.
Kazi
ya kwanza ambayo makocha hao watatakiwa kuifanya ni kuhakikisha wanaivusha
Stars kwenye
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “YANGA YAMGOMEA KOCHA WAKE KUINOA STARS.”
Post a Comment