Wednesday, September 30, 2015
HII NDIO SABABU YA STEWART HALL KUMUANZISHA BENCHI JOHN BOCCO LEO..
Do you like this story?
Kocha mkuu wa Azam FC Stewart Hall
amesema wakati kikosi chake kitakapokuwa kinapambana na Coastal Union leo
kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, nahodha wa kikosi hicho John Bocco
ataanzia benchi kwasababu anasumbuliwa na goti baada ya kuumia kwenye mchezo
ulipopita dhidi ya Mbeya City.
Mtandao huu umefanya mahojiano na
Stewart Hall ili kutaka kujua hali ya Bocco kisaikolojia na kama yuko tayari
kuendelea kucheza kwenye kikosi cha Azam kwenye michezo ya hivi karibuni
inayokikabili kikosi hicho.
“Nahodha wetu John Bocco ataanzia
benchi kwenye mchezo wa kesho, lakini kuanzia kwake benchi hakuhusiani na tukio
lililotokea kwenye mechi iliyopita bali anasumbuliwa na matatizo ya goti ambayo
alipata kwenye mechi iliyopita wakati tunacheza na Mbeya City”, amesema Hall.
“Tukio lililotokea kwenye mchezo
uliopita la mchezaji wa Mbeya City kumdhalilisha mchezaji wetu ni la aibu kubwa
na halifai kufanywa na mchezaji wa ngazi ya ligi kuu. Matokeo yake badala ya
watu kujadili mchezo wa Azam dhidi ya Mbeya City mchezo uliokuwa mkali na wenye
upinzani mkubwa, wamehama na kuanza kujadili tukio hilo ambalo ni la aibu”.
“Lakini tunashukuru kitendo hicho
kimeonekana na TFF wameshatoa kauli yao japo haikuwa rasmi kuhusu mchezaji
aliyehusika na udhalilishaji wa aibu kwa aina ya mchezaji mwenyewe ambae
amejiaibisha pia yeye pamoja na timu yake”.
“Club yetu inawataalamu wengi wa
kila aina pamoja na wanasaikolojia ambao tayari wamekaa na mchezaji na
kuzungumza nae, tunashukuru Bocco yuko vizuri na ametuhakikishia kuwa yuko
tayari kuendelea kucheza”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HII NDIO SABABU YA STEWART HALL KUMUANZISHA BENCHI JOHN BOCCO LEO..”
Post a Comment