Wednesday, September 30, 2015
JOB NDUGAI AMUUNGA MKONO EDWARD LOWASSA.
Do you like this story?
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kogwa kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), Job Ndugai, amesema iwapo atachaguliwa kuliongoza jimbo hilo
kwa awamu ya nne, atahakikisha anatatua mgogoro kati ya wakulima wa Wilaya ya
Kogwa na wafugaji wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
kwa mujibu gazeti la MwanaHALISI Online leo, Ndugai ambaye
pia ni Naibu Spika amesema: “Sababu kubwa iliyopelekea kukua kwa mgogoro huu ni
mzaha, ubinafsi na uzembe uliokuwa ukifanywa na baadhi ya viongozi wa serikali
wilayani Kiteto katika kusuruhisha mgogoro kati ya wafugaji na wakulma.”
“Iwapo nitapewa ridhaa ya kuiongoza Kogwa kipaumbele cha
kwanza ni kurejesha amani kati ya wakulima na wafuagaji katika wilaya za Kiteto
na Kogwa. Tutakaa chini na viongozi ili kutatua tatizo hili,” amesema Ndugai.
Mbali na Kauli hiyo, Ndugai pia anakubaliana na kauli ya
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa kuhusu kuunda tume ya maridhiano
itakayoshughulika migogoro ya wakulima na wafugaji ili kuondokana na matatizo
ambayo yamekuwa yakiwasumbua, iwapo atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano.
Lowassa alitoa kauli hiyo wiki iliyopita wakati wa mkutano
wa kampeni katika uwanja wa Soweto wilayani Kiteto.
“Wazo alilolitoa Lowassa ni zuri hasa kwa mtu yoyote
anayependa amani ipatikane. Ni aibu Watanzania kuchinjana. Viongozi
tutakaochaguliwa kutumikia wananchi ni lazima tukae chini ili kumaliza tataizo
hili. Tunahitaji kuwa na mipango, wala hatuhitaji kuwa na fedha za kigeni
kumaliza migogoro,” amesema Ndugai.
Mwaka 2014 Watanzania walishuhudia mauaji ya kutisha ya watu
10 wilayani Kiteto katika kile kinachotajwa ni mgogoro baina ya wafuagaji na
wakulima ambao wanahangaika kutumia eneo la ardhi kwa ajili ya mahitaji yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JOB NDUGAI AMUUNGA MKONO EDWARD LOWASSA.”
Post a Comment