Wednesday, September 30, 2015
NEC WAAPA KULA SAHANI MOJA NA WABAYA WA LOWASSA
Do you like this story?
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian
Lubuva ametoa ovyo kali na kuahidi kuwachukulia hatua za kisheria, wanasiasa na
wagombea wanaofanya kampeni chafu kwa kutaja majina ya watu, pamoja na
kuingilia kazi za NEC.
Anadai, amekuwa akishangwazwa na kitendo cha baadhi ya
wagombea kupanda majukwaani kuwasema vibaya wagombea wenzao na kuwakashifu
badala ya kutumia nafasi hiyo kwa kutangaza sera za chama na wagombea.
Hayo ameyasema Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya New
Afrika alipokutana na wawakilishi wa walemavu nchini ili kuzungumzia masuala
mbalimbali ya uchaguzi likiwemo la kuwapo utaratibu wa kupiga kura.
Kabla ya utaratibu wa upigaji kura kwa walemavu kutolewa,
Lubuva pia amevitaka vyama vya siasa kutokuwa na wasiwasi na NEC kama ilivyo
kwa baadhi ya vyama ambavyo vinaonekana kutoiamini tume hiyo na kuwataka
wanasiasa wanaona mwanya wa kuiba kura, wampe taarifa ili wazifanyie kazi.
“Kuna baadhi ya wanasiasa sitawataja lakini nawasikia
wakiwasisitiza wanachama wao kutoondoka katika vituo vya kupigia kura siku hiyo
kwa kigezo cha kulinda kura.
“Huo ni upotoshaji na ni kujisumbua, kwani hakuna kura
itakayoibiwa kila mtu akimaliza arudi kwao na kusubiri matokeo,” amesema
Lubuva.
Neye Kaimu Mkurugenzi wa NEC, Emmanuel Kawishe wakati akitoa
maelekezo kwa walemavu hao amesema, siku hiyo ya uchaguzi, walemavu wote
hawatakaa foleni bali watapita moja kwa moja sehemu ya kupigia kura.
Kawishe amesema kundi hilo na makundi maalumu likiwemo la
wazee, wajawazito hawatakaa foleni pia. Na kwa wale walemavu wa macho
wataruhusiwa kwenda na wasaidizi wao ndani ya chumba cha kupigia kura.
“Lakini tunawakumbusha tu makundi hayo ya walemavu wachague
wasaidizi wasiohusika na uongozi katika chama chochote na wala asiwe wakala wa
chama au Tume ili kuepusha ulaghai na wizi wa kura,” amesema Kawishe.
Pia amesema NEC inampango wa kuweka makaratasi maalumu ya
kuandikia kwa wale wenye ulemavi wa macho pamoja kuandika maandishi makubwa ya
wagombea ili kuwasaidia wenye matatizo ya kuona kama walemavu wa ngozi
(Albino).
“Nadhani tutakuwa tumezingatia maombi yenu kwenye mchakato
wa upigaji kura, tumeweka vituo katika maeneo rafiki kwenu na tumefanya hivyo,
vituo vyote 72,000 vilipo katika maeneo mazuri mtakayoweza kwenda,” amesema
Kawishe.
Amesema vituo vyote vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na
kufugwa saa 12:00 ambapo mawakala wote wanatakiwa kuwepo katika chumba cha
kupigia kura.
“Lakini kwa wakala ambaye hatakuwepo zoezi litaendelea kama
kawaida hatutasitisha zoezi ili kumsubiri,” amesema Kawishe.
Aidha, Mkurugenzi huyo ametoa ufafanuzi juu ya Majimbo na
Kata zote ambazo vyama vya siasa vimepoteza wagombea wao, Oktoba 12 hadi
Novemba 22 vyama vinatakiwa kumteua mgombea mwingine ili kuziba pengo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ NEC WAAPA KULA SAHANI MOJA NA WABAYA WA LOWASSA”
Post a Comment