Wednesday, September 30, 2015
KIKONGWE MIAKA 100 AMTABIRIA MAGUFULI.
Do you like this story?
Dustan Shekidele, Morogoro.
UTABIRI! Wakati taasisi
mbalimbali zisizo za kiserikali zikitoa matokeo ya utafiti katika
kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu mwezi ujao, kikongwe mmoja, Kete Abdallah
mwenye umri wa miaka 100, amemtabiria ushindi mgombea urais wa CCM, Dk. John
Magufuli.
Bibi huyo alitoa utabiri huo wiki iliyopita
wakati wa sherehe yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa iliyoandaliwa na wajukuu na
vilembwe wake na kufanyika nyumbani kwake, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wajukuu zake, Dustan, alisema
alimkuta bibi yake akiwa amelala kitandani akiwa amekumbatia redio na
alipomuuliza sababu ya kuwa hivyo, alidai anafuatilia habari za mgombea huyo,
kwani anaamini atashinda na endapo ataamka salama siku hiyo, atampatia kura
yake ya ndiyo.
"Unajua ukubwa dawa, najua kila mtu ana
chama chake siwezi kuwaingilia, lakini ninawashauri viongozi wangu wa CCM,
uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu, upinzani umekuwa na nguvu,” alisema bibi huyo
na kuwashauri viongozi wa CCM kutembelea majumbani na mahospitalini kuwabaini
makada wa CCM ambao hawataweza kutoka kwenda kupiga kura.
Mmoja wa vilembwe wa bibi huyo, Tumaini
Shekidele akisoma risala kwenye sherehe hiyo, alisema bibi huyo alizaliwa
Septemba 27, 1915 katika Tarafa ya Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga na
kwamba hadi sasa ana wajukuu na vilembwe 302.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIKONGWE MIAKA 100 AMTABIRIA MAGUFULI.”
Post a Comment