Wednesday, September 30, 2015

NYOSSO APEWA KIFUNGO NA FAINI JUU BAADA YA KUMDHALILISHA BOCCO




Kikao cha Kamati ya nidhamu ya TFF kilichokutana ndani ya saa 72, kimefungia nahodha wa Mbeya City, Juma Said Nyosso kucheza soka kwa miaka miwili.


Pamoja na miaka hiyo miwili, Nyosso ametozwa faini ya Sh milioni mbili kutokana na kitendo chake cha kumshika makalio nahodha wa Azam FC, John Bocco.


Hii ni mara ya pili kwa Nyosso kushiriki katika tukio, mara ya kwanza alimtomasa Elius Maguli wakati akiichezea Simba.


Kutokana na picha ilivyochapishwa kwenye gazeti la Championi na SALEHJEMBE akafungiwa kucheza mechi nane.


Baada ya hapo, Nyosso aliwaomba radhi Watanzania pamoja na wapenda soka wote, lakini bado amerudia.

 

0 Responses to “ NYOSSO APEWA KIFUNGO NA FAINI JUU BAADA YA KUMDHALILISHA BOCCO”

Post a Comment

More to Read